2014-07-19 10:30:41

Onesho linalokusudia kuibua na kukuza vipaji!


Baraza la Maaskofu Katoliki Afrika ya Kusini kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Wayesuit, Jimbo kuu la Johanesburg, wameandaa onesho la vyombo vya mawasiliano ya Kanisa Afrika ya Kusini. Onesho hili ambalo litafanyika Jumamosi tarehe 26 Julai 2014 linaongozwa na kauli mbiu "Njoo ukuze vipaji vyako vya mawasiliano".

Walengwa wakuu ni wanafunzi wa shule za sekondari, taasisi za elimu ya juu pamoja na vyuo vikuu nchini Afrika ya Kusini, bila kuwasahau wadau katika ulimwengu wa mawasiliano ya Jamii kutoka katika Majimbo na Parokia mbali mbali mbali nchini Afrika ya Kusini.

Vyombo vya mawasiliano ya Jamii vinavyomilikiwa na kuendeshwa na Kanisa Katoliki Afrika ya Kusini, vitafanya onesho ili kuwashirikisha waamini na watu wote wenye mapenzi mema uzoefu na mang'amuzi ya Kanisa katika mchakato wa Uinjilishaji Mpya. Hawa ni watu wanaofanya kazi katika mitandao ya kijamii, Radio, Luninga, Magazeti na Majarida mbali mbali. Watu watakaoshiriki katika onesho ili ambalo pia linaweza kuwa ni msaada mkubwa kwa vijana kutambua na hatimaye kukuza vipaji vyao, watafundishwa nadharia asubuhi na jioni, wataweka katika vitendo yale waliyojifunza!









All the contents on this site are copyrighted ©.