Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa sana na taarifa kuhusu kutunguliwa kwa Ndege
ya Shirika la Ndege la Malaysia, Alhamisi tarehe 17 Julai, katika eneo la Ukraine
ambayo kwa sasa imegeuka kuwa ni uwanja wa vita na kinzani. Baba Mtakatifu anawakumbuka
na kuwaombea abiria 298 waliofariki dunia katika ajali hii pamoja na wote walioguswa
na msiba huu mkubwa.
Baba Mtakatifu anawasihi wahusika wa mgogoro wa vita
nchini Ukraine kusitisha vita na kuanza kujielekeza zaidi katika njia za majadiliano,
ili kujenga na kudumisha misingi ya haki na amani sanjari na kuokoa maisha ya watu
wasiokuwa na hatia yanayoendelea kupotea kutokana na vita!