2014-07-18 11:22:38

Askofu mkuu Telesphore Mpundu ndiye "Jembe jipya" la Baraza la Maaskofu Katoliki Zambia!


Baraza la Maaskofu Katoliki Zambia katika mkutano wake mkuu uliohitimishwa hivi karibuni, umemchagua kwa mara nyingine tena Askofu mkuu Telesphore George Mpundu kuwa Rais Mpya wa Baraza la Maaskofu Katoliki Zambia. Askofu mkuu Mpundu anachukua nafasi ya Askofu mkuu Ignatius Chama wa Jimbo kuu Katoliki la Kasama na msimamizi wa kitume wa Jimbo Katoliki la Mpika, Zambia.

Hii ni mara ya tatu kwa Askofu mkuu Mpundu kuchaguliwa kuliongoza Baraza la Maaskofu Katoliki Zambia kama Rais wake. Itakumbukwa kwamba, kwa mara ya kwanza alichaguliwa kunako mwaka 1993 na kuliongoza Baraza kwa awamu mbili mfululizo hadi kunako mwaka 1999. Kunako mwaka 2002 akachaguliwa tena na kumaliza muda wake wa uongozi mwaka 2008.

Baraza la Maaskofu Katoliki Zambia kadiri ya taarifa ya Katibu mkuu wa Baraza hili Padre Cleophas Lungu inasema kwamba, Makamu wa Rais amechaguliwa Askofu Alick Banda wa Jimbo Katoliki la Ndola.







All the contents on this site are copyrighted ©.