2014-07-17 11:11:50

Tangazeni utakatifu na ukuu wa Familia!


Kuna umati mkubwa wa waamini ambao haufahamu fika mafundisho ya Kanisa Katoliki kuhusu maisha ya ndoa na familia. Dhamana na utume wa Kanisa ni kuwatangazia watu Habari Njema ya Wokovu kwa kuwakirimia watu fursa ya kukutana na Yesu Mkombozi wa dunia, ili aweze kuwakirimia utimilifu wa maisha. RealAudioMP3

Yesu Kristo anaendelea kuokoa Familia kwa njia ya Kanisa, kumbe, Kanisa katika mapambazuko ya Millenia ya tatu ya Ukristo linachangamotishwa kutangaza kuhusu ukuu na utakatifu wa maisha, urithi mkubwa uliochwa na Mtakatifu Yohane Paulo II katika Waraka wake wa kichungaji, Familiaris Consortio, Uwajibikaji wa Familia ya Kikristo. Ni wajibu kwa waamini kuwashirikisha jirani zao Injili ya Furaha.

Kanisa litaendelea kulinda, kutetea na kudumisha misingi bora ya maisha ya ndoa na familia, kwani familia ni kitovu cha ustawi na maendeleo ya mwanadamu. Hapa kuna haja ya kuwafundisha watu Katekesi juu ya upendo wa binadamu!







All the contents on this site are copyrighted ©.