Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Argentina walioshiriki kwenye mashindano ya Kombe la
Dunia nchini Brazil kwa mwaka 2014 wamemzawadia Baba Mtakatifu Francisko jezi iliyopambwa
kwa sahihi za wachezaji kutoka Argentina. Wachezaji hawa kutoka Argentina hata baada
ya kuchalazwa bao moja kwa nunge na Wajerumani, wanamshukuru Baba Mtakatifu Francisko
kwa kuwakumbuka na kuwaombea walipokuwa wanashiriki katika mashindano ya Kombe la
Dunia, huko Brazil.
Picha kubwa ya Baba Mtakatifu akiwa na wachezaji wa timu
ya taifa ya Argentina ilipambwa katika eneo ambalo wanamichezo hawa walikuwa wanafanyia
mazoezi yao nchini Brazil. Hii ni picha waliyopiga na Baba Mtakatifu wakati walipomtembelea
mjini Vatican hivi karibuni.