2014-07-16 12:40:00

Askofu mkuu Bernardito C. Auza, ateuliwa kuwa Mwakilishi wa Vatican kwa Mashirika ya Nchi za Amerika


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Bernardito Cleopas Auza kuwa Mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Mashirika ya Nchi za Amerika, O.A.S. Wakati huo huo, ataendelea kuwa ni Mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Umoja wa Mataifa, huko New York, Marekani.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Auza alizaliwa kunako tarehe 10 Juni 1959 huko Tallibon, nchini Ufilippini. Baada ya kuhitimu masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapadrishwa kunako tarehe 29 Juni 1985 na Askofu Daniel Francis Walsh. Tarehe 8 Mei 2008 akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Haiti. Akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu hapo tarehe 3 Julai 2008 na Kardinali Tarcisio Bertone, aliyekuwa Katibu mkuu wa Vatican kwa wakati ule.







All the contents on this site are copyrighted ©.