2014-07-14 09:30:23

Mwenyeheri mtarajiwa Askofu Alvaro del Portillo!


Zaidi ya watu laki moja kutoka katika nchi sabini wanatarajiwa kuhudhuria katika Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kumtangaza Mtumishi wa Mungu Askofu Alvaro del Portillo, mwandamizi wa kwanza wa Mtakatifu Josemaria Escrivà de Balaguer katika kuliongoza Shirika la Kazi ya Mungu, maarufu kama “Opus Dei” kuwa Mwenyeheri. RealAudioMP3

Ibada itaadhimishwa katika Jimbo kuu la Madrid, hapo tarehe 27 Septemba 2014. Taarifa hii imetolewa na kamati ya maandalizi ya kumtangaza Mtumishi wa Mungu del Portillo kuwa Mwenyeheri sanjari na kalenda ya maadhimisho haya. Itakumbukwa kwamba, Jimbo kuu la Madrid ndipo mahali alipozaliwa Mtumishi wa Mungu del Potillo, lakini sehemu kubwa ya maisha yake alikuwa mjini Roma, yaani tangu mwaka 1943 hadi mwaka 1994, alipofikwa na mauti kadiri ya mpango wa Mungu.

Masalia ya mwili wa Mtumishi wa Mungu del Portillo yamehifadhiwa kwenye Kanisa kuu la Bikira Maria Mama wa amani, lililoko mjini Roma. Baada ya maadhimisho haya hapo tarehe 29 Septemba na tarehe 2 Oktoba, washiriki wengi katika matukio haya watarejea mjini Roma na kuendelea kumwimbia Mwenyezi Mungu utenzi wa sifa na shukrani kwa kumjalia Mtumishi wake del Portllo kutangazwa kuwa Mwenyeheri, mfano wa kuigwa katika utakatifu wa maisha!








All the contents on this site are copyrighted ©.