2014-07-12 15:59:25

Michezo iwe ni fursa ya ujenzi wa utamaduni wa kukutana!


Mashindano ya Kombe la Dunia yanafikia ukingoni kwa kuzipambanisha timu za Argentina na Ujerumani. Hadi kufikia hapa, wanamichezo wametoana jasho kweli kweli na wala si utani! Kuna watu wamesafiri kutoka sehemu mbali mbali za dunia ili kwenda kuangalia jinsi wanamichezo walivyokuwa wanatandaza kabumbu ya nguvu!

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anasema kwamba, mashindano ya Kombe la Dunia huko Brazil kwa mwaka 2014 yamekuwatanisha watu kutoka katika mataifa na dini mbali mbali. Kutokana na mantiki hii, michezo inaweza kuwa ni fursa ya kukuza na kuimarisha utamaduni wa watu kukutana!







All the contents on this site are copyrighted ©.