Serikali ya DRC imekanusha uwepo wa mchakato unaotaka kufanya mabadiliko katika Katiba
ya Nchi ambayo kimsingi ni sheria mama ili kumwezesha Rais Joseph Kabila kuwania tena
madaraka katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini humo mwaka 2016.
Itakumbukwa
kwamba, Baraza la Maaskofu Katoliki DRC liliona kwamba jitihada zozote za kutaka kufanya
marekebisho katika Katiba zinaweza kutibua mustakabali wa wananchi wa DRC. Maaskofu
wanataka kuona uchaguzi nchini humo unakuwa: huru, kweli na haki. Ni wajibu wa wanasiasa
kusimamia mafao ya wengi, ustawi na maendeleo ya wananchi wa DRC.