(Vatican Radio / PCCS) Baba Mtakatifu Francisco, ameonyesha kufurahia juhudi za
vyombo vya mawasiliano Vatican katika huduma zake za kuimarisha uwepo wa vyombo
hivyo katika ulimwengu wa digital. Papa alionyesha furaha hiyo, siku ya Jumatatu,wakati
akitazama toleo la ukurasa mwingine mpya, katika simu ya mkononi “lilioitwa “The
Pope App", kama ilivyobuniwa na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mawasiliano Jamii.
Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mawasiliano Jamii, Askofu Mkuu Claudio
Celli, akifuatana na mratibu wa juhudi hizo, Thaddeus Jones, walikutana na Papa kuonyesha
sifa za ukurasa huo, ambao tangu tarehe 4 Julai ulianza kupatikana katika mitandao
ya iTunes na Google, katika lugha tano. Pope App 2.0 inapatikana bure na inaweza
kunakiriwa bure au kuchotwa bure kwenye vifaa Apple na Android. Na kwa kuwezeshwa
na News.va, inatoa taarifa na habari za hivi karibuni juu ya Papa, kama zinavyo
tolewa na vyombo vya habari vya Vatican ikiwemo Vatican Radio.
Lengo la
mradi huu ni kurahisisha zaidi upatikanaji wa habari sahihi za Vatican. Askofu Mkuu
Celli, alieleza na kuongeza pia inaruhusu watu kuwa karibu zaidi Papa, katika huduma
yake ya kichungaji na ujumbe wake wa upendo wa Mungu.
Akizungumza na Gazeti
la L’0sservatore Romano juu ya Juhudi katika mtazamo kutunza jadi na ubunifu mpya
, katika ulimwengu wa Mawasiliano , anasema, katika hatua kubwa za maendeleo makubwa
katika mawasiliano ya digital, "Kanisa kwa wakati huu, kwa hakika haliwezi kujitenga
na kubaki katika mawasiliano ya jadi ya redio, televisheni na magazeti. Ni hakika
Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mawasiliano ya Jamii, aliendelea kueleza, Kanisa
haliwezi kufungia nje hatua za maendeleo katika njia hii ya mawasiliano, ingawa haina
maana kupoteza hisi zake za nguvu , katika uwajibikaji wa kutunza uadilifu katika
mazingira ya teknolojia mpya.
Na ndiyo maana, pamoja na Papa Francisco, kuendelea
kuonyesha kuwa karibu sana na mfumo wa jadi wa mawasiliano, pia hajiweki mbali na
mifumo ya sasa katika mawasiliano jamii . Yeye anapenda kuzungumza na watu, katika
kila uwezekano, hata mawasiliano ya simu moja kwa moja kwa wahusika badala ya kutegemea
tu weledi wa maelezo katika mtandao; na hajaacha utamaduni wa kuandika barua kwa
mkono wake mwenyewe. Lakini pamoja na hilo, hutumia njia za kisasa kama kutuma ujumbe
kwa makundi ya watu, ambao huonana nao ana kwa ana kupitia mtandao wa video , ambayo
hutoa nafasi za kusikilizana na kubadilishana mawazo kama vile wako sehemu moja.
Na pia muda wote yuko tayari kuzungumza na waandishi wa habari, vyombo vya habari,
magazeti au mitandao ya televisheni, na huwa tayari kufanya mahojiano, na hajamkatalia
mtu yeyote.
Maneno ya Papa daima ni wazi, halisi na moja kwa moja na si ya
mkato wala kuzunguka mbuyu. Na huheshimu mahojiano hasa na wazee ambao pengine kwao
si rahisi kuikubali teknolojia mpya au kutumia vifaa vya kisasa au lugha ya tarakimu
katka ulimwengu wa mitandao ya kijamii. Watu ambao bado wanathamini zaidi habari
zilizochapishwa katika magazeti, au kutangazwa katika redio na televisheni. Lakini
pia Kanisa haliwezi kubaki limejifungia tu katika njia hizo za kijadi, kwani ni muhimu
likatembea pamoja na teknolojia Mpya. Na Papa Francisco anajua na anaruhusu hilo,
ameeleza Askofu Mkuu Celli katika mahojiano na gazeti la L'Osservatore Romano.