Tume ya kutetea watoto dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia yakutana Vatican
Tume ya Kipapa kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto dhidi ya manyanayso ya kijinsia, ilifanya
kikao chake Jumapili hadi Jumatatu ( 6-7Julai 2014 ), katika jengo la Domus Sanctae
Marthae, chini ya uratibu wa Kardinali Sean Patrick O'Malley, OFM Cap., Kwa kushirikiana
na Msgr. Robert Oliver .
Padre Federico Lombardi, Mkuu wa Ofisi ya Habari
ya Vatican, akitoa muhtasari wa kikao hicho cha siku mbili , alitaja kikao hicho kilifanya
majadiliano yake kwa kuzingatia mada zifuatazo : - Mapendekezo kwa ajili ya uchaguzi
na uteuzi wa wajumbe wapya , kwa lengo la kuishirikisha tume katika uwakilishi mpana
zaidi kutoka maeneo mbalimbali ya kijiografia. - Katiba ya Tume. - Haja ya
kuanzisha ofisi za utendaji za Tume. - Uwezekano wa kuandaa vikundi kazi juu
ya mada maalum kwa kushirikiana na ya wataalamu na taasisi nyingine.
Kikao
kilikamilika kwa kutaja kikao kijacho , kitafanyika mwezi wa Oktoba. Ni matumaini
ya Tume kwamba wajumbe wapya walio chaguliwa au kuteuliwa wataweza kuhudhuria kikao
. Aidha kikao hicho, kilitoa angalisho maalum katika maandalizi ya wahanga kadhaa
wa madhulumu ya kinjisia yaliyofanywa na viongozi wa Kanisa, kukutana na Papa Francisco,
kama ilivyokuwa imepangwa.
Wahanga hao waliowasili katika nyumba ya wageni
ya Mtakatifu Marta ya mjini Vatican, wakati wa mlo wa mchana, Papa alijitokeza na
kuwasalimia kwa hotuba fupi . Wahanga hao walikuwa ni watu wazima sita , wanaume
watatu na wanawake watatu, kutoka UjerumanI , Ireland, na Uingereza, na kila mwathirika
alikuwa amesindikizwa na familia yake au rafiki yake.
Tukio hili ni mwaliko
uliotolewa na Cardinal O'Malley kwa nchi kadhaa ambapo Kanisa limeunda mfumo maalum
kuhusu waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia. Na Washiriki waathirika walipewa mwaliko
wa kukutana na Papa. Mapema Jumatatu Papa alitolea Ibada ya Misa kwa ajili yao katika
Kanisa dogo la Mtakatifu Marthae, na wahanga walihudhuria pia na wote waliokuwa
wameandamana nao, pia wajumbe wa Tume kwa ajili ya ulinzi wa watoto, na idadi ndogo
ya waamini wengine. Nia kuu ya Ibada hiyo ikiwa kwa ajili ya haki na amani.
Baada
ya Misa, Papa alisalimu kila aliyeshiriki katika Ibada hii . Baada ya kifungua kinywa,
Papa , alifanya a majadiliano binafsi katika chumba cha faragha ndani Jengo la Domus
Sanctae Marthae na kila mhanga akiwa na wale walioandamana naye , mmoja baada ya
mwingine. Majadiliano yaliyodumu ilidumu tangu saa tatu hadi saa sita na nusu za
mchana.
Washiriki, baada ya majadiliano, walionyesha hisia zao na kuridhika
baada ya kusikilizwa na Papa na jinsi alivyoonyesha kujali na tahadhari inayotolewa
. Papa alionyesha wazi kwamba, kumsikiliza mtu, husaidia kuelewa na kuandaa njia ya
kurejesha imani, kuponya majeraha, na kufungua uwezekano wa maridhiano na Mungu na
Kanisa.