2014-07-08 15:53:18

Mafanikio yaonekana katika mageuzi mapya ya Benki ya Vatican.


Benki ya Vatican, ambayo ni Taasisi ya Jimbo la Papa kwa ajili ya masuala ya kiuchumi na fedha (IOR ) imechapisha mizania ya matokeo ya bajeti ya 2013,na mizania ya kipindi cha nusu mwaka 2014 na kutangaza mwanzo wa awamu ya pili ya mageuzi katika taasisi hiyo. Katika Riporti iliytolewa Jumanne Julai 8, 2014, inaonyesha katika mwaka 2013, ambao ulikuwa ni mwaka wa kuimarisha uwazi katika IOR, ilifunga jumla ya akaunti elfu tatu zisizo eleweka za wateja mbalimbali.Taasisi hiyo ambayo pia imetaja kwa mwaka uliopita 2013, ilitenga jumla ya Euro 54, Milioni kwa bajeti za Jimbo la Papa.
IOR imetoa taarifa ya kina yenye kuwa na habari za hivi karibuni katika matokeo ya utendaji yaliyo patikana katika kipindi cha mageuzi Awamu ya kwanza ya Taasisi hiyo. Ripoti hiyo pia inazidua Mkakati wa utendaji kwa Awamu ya Pili, kwa ushirikiano wa Taasisi ya mpya za utawala kiuchumi Vatican, utakao dhaminishwa Bodi mpya na usimamizi wa wafanyakazi wateule, na itafanya kazi katika muundo mpya utawala.
Mwenyekiti wa a Bodi ya IOR, Ernst Von FREYBERG , anasema, masuala ya Uchumi na Fedha katika Jimbo la Papa, kama ilivyo elezwa awali Mwezi Mei 2013, IOR, utendaji wake, umelenga zaidi katika kutengeneza kanuni na sheria imara za fedha kwa ajili ya usalama zaidi na uwazi, ili Baba Mtakatifu aweze kuwa na chaguzi zaidi wakati wa kuamua juu ya hatma ya IOR.

Na kwamba utendaji huo umeweza kuweka msingi mpya , kwa ajili ya usimamizi wa IOR, kama huduma ya kweli ya kipekee katika ulimwengu wa fedha Katoliki. Pamoja na juhudi zinazofanywa katika kuboresha usimamizi wa ndani, IOR imekuwa na utendaji mzuri kwa wateja wake, kati ya wote kwa jimbo Takatifu. Na kwamba katika kipindi cha nusu mwaka cha 2014, kimekuwa na mafanikio mazuri, ambayo inathibitisha juhudi na nguvu mpya za wanafanya kazi wote wa IOR .

Ripoti hiyo inaendelea kuonyesha, Mizania ya Taarifa za fedha, iliyofanyika kwa misingi ya Viwango Uhasibu vya kimataifa, IFRS) na kukaguliwa na Deloitte & Touche SpA, na kutoa taarifa ya marekebisho ya bajeti ya 2013, ripoti ya mwaka ya Taasisi ilichapishwa Oktoba 1, 2013 kama sehemu ya Mpango wa mradi mkubwa ulizindua mwaka 2013 na malengo ya kuonyesha dhamira, shughuli na utendaji wa kifedha wa IOR, katika kutoa taarifa mara kwa mara juu ya maendeleo, katika suala la mageuzi. Ripoti ya mwaka 2013, alifuatana na ripoti ya ukaguzi, na kuchapishwa Julai 15, 2014 katika tovuti ya IOR (www.ior.va). Mwaka 2013.

Matokeo ya nusu ya kwanza ya 2014 kimsingi utendaji yamekuwa ya kuridhisha ikionyesha uwepo wa kumbukumbu faida ya EUR 57,400,000, na gharama za uendeshaji kupungua ikilinganishwa na mwaka 2013. Haya ni matokeo ya shughuli za kawaida za Taasisi IOR, pamoja na mchakato wa mageuzi katika Taasisi ya kazi za Mashirika Katoliki, , Shirika la Sixtus V, Posta ya Vatican,, na kumbi za Vatican Chini ya Mamlaka ya Udhibiti wa masuala ya fedha (AIF)

Mwenyekiti Bodi ya IOR, Ernst Con Freyberg, akizungumza na Redio Vatican juu ya ripoti hii pia ametoa ufafanuzi kwamba, tangu awe mwenyekiti 2013, IOR, imefunga jumla ya akauntiza benki 3000 kati yake 2600 ikiwa ni zile zisizo hai, ambazo nyingi zikiwa ni waseminaristi wanaofika Roma kwa ajili ya masomo , na wanapokamilisha masomo yao huondoka bila kujifunga. Wengi wao wakiacha kima cha chini cha kufungua akaunti au kuwa na deni.

Na pia wamefunga jumla ya akaunti 400 za walei, watu ambao walikuwa na haki ya kuwa na akaunti katika benki ya Vatican kwa mujibu wa sheria za zamani , lakini kwa sheria na mfumo wa sasa waliombwa kufngua akaunti zao katika benk za nchi ya Italia. Hatua iliyofanyika kwa mujibu wa sheria, kama walivyokuwa wametolea maamuzi mwezi Julai mwaka jana, yanayo lenga benki ya Vatican ibaki kuwa huduma ya kibenki kwa kanisa katika maana huduma kwa mashirika , Majimbo, Mapadre, wafanyakazi wa Vatican na Jimbo la Papa , pia Parokia. Na hiyo ndiyo sababu ya kufungwa kwa akaunti za watu wasiokuwa na mahusiano ya moja kwa moja na Vatican au Jimbo la Papa.








All the contents on this site are copyrighted ©.