2014-07-07 09:55:06

Wakimbizi wana haki zote za binadamu, na si tu katika misaada


Watu wanaokimbia makazi kwa sababu za kusalimisha maisha , wana haki na wajibu wote wa binadamu ,na si tu katika malengo ya kupata misaada. Ni Ujumbe wa Askofu Mkuu , Silvano Maria Tomasi, Mtazamaji wa Kudumu wa Jimbo Takatifu katika Ofisi za Umoja wa Mataifa za Geneva, wakati akizungumza katika Kikao cha 60 cha Kamati ya Kudumu ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Kuhudumia Wakimbizi. Hotuba yake ilizingatia hali halisi ya takwimu za wakimbizi zinazo ongezeka kila siku ,sasa ikielekea karibia milioni 50 ya watu waliokimbia makazi yao. Idadi hii inatajwa ni kubwa zaidi ya wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia . Na hivyo alisisitiza, haja ya kulinda "haki na heshima ya binadamu" kwa sababu "ulinzi wa uhuru wa mtu binafsi unapaswa kupewa kipaumbele cha kwanza, juu ya masuala yote ya ulinzi na usalama kiserikali.


Hivyo, Ujumbe wa Askofu Mkuu Tomasi, umetoa mwaliko si tu katika kufikiria mapokezi ya wakimbizi bila kujali uhuru na heshima yao binafsi , lakini ni kuwapokea kwa heshima na uhuru binafsi kama sehemu ya uwajibikaji wa ulimwengu wa kisiasa, kitaifa na kimataifa. Suala la wakimbizi, aliendelea, ni lazima kushughulikiwa na sera imara za kulinda usalama wa taifa ambazo lakini ni taratibu nyepesi katika kuvuka mpaka, pia kwa ajili ya upatikanaji wa hifadhi kwa urahisi zaidi , na hasa uwezekano kuwa na nafasi zaidi za makazi bora kwa wakimbizi na wahamiaji. Alieleza kwa kuangalisha barani Ulaya, akisema hasa, ni muhimu kuwa na mkakati wa pamoja, ili kwamba nchi zinazo kuwa mlango mwepesi wa kukimbiliwa na wakimbizi, zisiachiwe mzigo huo wa kuwapokea na kuhifadhi wakimbizi hao, kabla ya kusambaa katika mataifa tofauti.


Aidha hotuba yake , ilitumaini kwamba, elimu na mwamko wa umma kuhusu wajibu wa pamoja juu ya sababu za migogoro na utafutaji wa ufumbuzi kwa njia ya amani, litakuwa ni jukumu la jamii, katika kuitikia wito wa kushiriki kwa huruma na mshikamano, katika kutoa mchango wa kila mmoja kwa ajili ya utendaji wenye kuhakikisha kuwa, wahamiaji wa kulazimishwa wanatazamwa katika mtazamo mpana, wa umoja madhubuti na Mshikamano wa kuheshimu maisha na heshima ya binadamu , ili kuondoa mzizi wa sababu za mateso yanayo sababisha watu kukimbia au kuhama makazi yao au nchi.








All the contents on this site are copyrighted ©.