2014-07-07 09:58:27

Sr. Melone ateuliwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kipapa!


Profesa Mary Melone, mtawa mwenye umri wa miaka 50 ameteuliwa kuwa ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Antonianum kilichoko mjini Roma. Huyu ni mtawa kutoka Shirika la Wafranciskan ambaye anaweka historia ya kuwa ni mtawa wa kwanza kuteuliwa kuongoza Chuo Kikuu cha Kipapa. Ni mtaalam wa masuala ya elimu na taalimungu katika mafundisho tanzu ya Kanisa.

Ni Jalimu aliyebobea na kwa miaka kadhaa amefundisha chuoni hapo na ni mwandishi wa vitabu, majarida na makala mbali mbali. Mtawa aliyebobea katika kuhariri vitabu mbali mbali. Professa Melone atakiongoza Chuo Kikuu cha Kipapa cha Antonianum kuanzia mwaka 2014 hadi mwaka 2017.







All the contents on this site are copyrighted ©.