2014-07-07 08:32:44

Njooni kwangu nyote nami nitawapumzisha Yesu anaita leo.


Jumapili wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Francisco, alirudia mwaliko wa Yesu kwa watu wote, “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha" (Mt 11:28).

Yesu alitoa mwaliko huo kwa maelfu ya watu , waliokutana naye kila siku katika ya mitaa ya Galilaya, watu wengi wa kawaida , masikini, wagonjwa, wenye dhambi, watu wanyonge, watu ambamo daima walifuatana naye kusikiliza neno lake - neno la matumaini alilolitoa lenye kuwa na uwezo hata kwa kugusa upinde wa nguo yake. Yesu mwenyewe alikutana na umati huu wa watu, walio hoi na wenye wasiwasi kama kondoo wasio na mchungaji (. Mt 9:35-36). Alitangaza Ufalme wa Mungu, akiwaponya wengi kimwili na kiroho. Kama ilivyo kuwa wakati ule pia leo anawaita wote mwenyewe: "Njooni kwangu nyote," ahadi ya neema na faraja.

Papa akihutubia umati wa mahujaji na wageni waliofika kumsiliza wakati wa sala ya Malaika wa Bwana , katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, aliendelea kufafanua juu ya mwaliko huu Yesu kwa nyakati hizi, akisema, mwaliko ya Bwana na si tu wale waliolemewa na matatizo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Lakini pia hata kwa wale ambao , ingawa wanavyo vyote vya dunia hii , bado wanakabiliwa na utupu wa moyo. Yesu anaahidi kutoa kiburudisho kwa watu wote, na kuongeza kuwa, kuna, hata hivyo, pia mwaliko, ambayo ni kama amri: 'Jifungeni nira yangu na mjifunze kutoka kwangu, maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo” . Papa kisha alieleza maana ya “ nira ya Bwana” kwamba ni kubeba matatizo ya wengine kwa upendo wa kidugu.

Baba Mtakatifu aliwaambia waamini, "Mara baada ya kumepokea neema na faraja ya Kristo, tumeitwa kwa upande wetu pia kuwa neema na faraja kwa ajili ya ndugu na dada zetu, pamoja na maskini, kwa kuwa na tabia ya unyenyekevu, kwa kumwiga Bwana. Ni kuwafikia watu wote wake kwa waume , ambao wengi wao wamezidiwa na hali ya umaskini katika vyote, kiroho na kihali . Papa alitahadharisha hali ngumu ya maisha kwa wakati mwingine humtia mtu upofu wa kushindwa kuona mahali pa kufaa kuegemeza maisha. Aliendelea kusema, katika mataifa maskini, kama ilivyo pia katika nchi tajiri, kuna watu wengi walio hoi na wenye wasiwasi , walio chini ya uzito mashinikizo ya maisha, ingawa uzito hutofautiana.

Pembezoni mwa jamii kuna wanaume na wanawake wengi , waliomezwa na umaskini, pia ya kutoridhika maisha na hata kuchanganyikiwa. Wengi wanalazimika kuhama kutoka katika nchi yao, kuhatarisha maisha yake mwenyewe. Wengi zaidi kila siku hubeba uzito wa mfumo wa uchumi wa bwanyenye, usiyo weza kuvumilika, unaowekwa na watu wachache, wasiotaka kuiondoa nira hiyo. Lakini yafaa kukumbuka kwamba, kwa kila mmoja , kuna Baba aliye mbinguni, ambaye leo hii Yesu anasema, "Njooni kwangu, ninyi nyote."


Mwisho wa hotuba yake , Papa aliwaalika wote kujiweka chini ya ulinzi na maombezi ya Mama Bikira Maria, ili kwa njia ya mwanga wa imani, ushuhuda wa maisha katika Kristo , uweze kuwa faraja kwa wale ambao wanahitaji msaada, huruma na matumaini. Baada ya sala ya Malaika wa Bwana Papa Francisco alisalimia katika lugha mbalimbali, na kuzitaja Parokia mbalimbali zilizofika kwa ajili ya hija fupi Vatican, na kumsikiliza.








All the contents on this site are copyrighted ©.