2014-07-07 08:57:37

Lampedusa yaikumbuka Ziara ya Papa Francisco.


Vatican Radio) Papa Francisco, Jumapili alituma Ujumbe wake katika kisiwa cha Lampendusa, ambacho kinafanya kumbukumbu ya kutimia mwaka mmoja tangu alipofanya ziara yake ya kwanza ya kichungaji katika kisiwa hicho tarehe 8 Julai 2013. Kisiwa cha Lampedusa, ni kituo kikubwa cha wakimbizi na wahamiaji toka Afrika Kaskazini wanao ingia Ulaya kwa kupitia njia za panya, kuivuka bahari ya Mediterrania bila idhini.

Ujumbe wa Papa unaowalenga wakazi wote wa Lampedusa , umetumwa kwa Askofu Mkuu Francesko Montenegro wa jimbo kuu ya Agrigento, ambamo Lampedusa ni sehemu yake. Ujumbe unaohamasisha Wakristo na watu wote wenye mapenzi mema, kuendeleza moyo wa ukarimu, kusaidia wahitaji wote, bila kuhesabu gharama, bila kuwa hofu ya kupungukiwa , ila kwa kuongeza huruma na ufahamu wa mateso ya watu hao wanapo wainulia macho. Baba Mtakatifu anaendelea kuonyesha matumaini yake kwamba, taasisi husika, hasa katika ngazi ya Ulaya, zitaweza kuwa jasiri na karimu katika kusaidia wakimbizi.

Kwa ajili hii , Jumapili 6 Julai, Kardinali Antonio Maria Veglia, aliongoza Ibada ya Misa katika Parokia ya Matakatifu Gerlando, Lampedusa .

Homilia ya Kardinali Veglia ililenga zaidi katika maneno ya Papa Francisco , “Ndugu yako yuko wapi? aliyoyatoa mwaka mmoja uliopita, maneno kutoka kitabu cha Mwanzo. Swali hili lililosikika dunia nzima, wakati ikifuatiliwa kwa makini, ziara ya Papa katika kisiwa cha Lampedusa, ambayo sasa imekuwa rejea katika mjadala juu ya uhamiaji.

Swali hili "Yu wapi ndugu yako?" ni swali ambalo Mungu kwa mara ingine ameliweka tena mbele yetu , kama ilivyokuwa mwanzo wa historia ya binadamu, ili kila mmoja aone wajibu wake katika kuyalinda maisha ya wengine. Ni swali kuhusu wajibu wetu juu ya hatima ya watu wengi , walio kata tamaa ambao kwa njia mbalimbali wanatafuta kuokoa maisha yao, kwa njia za hatari za mitumbwi inayotazamiwa kutoa tumaini, ambayo imekuwa ni njia ya mauti, kama Papa Francis alivyo sema katika hotuba yake mwaka jana.

Kardinali Veglia amesema, Swali hili lililotolewa na Papa mwaka mmoja uliopita, katika kweli halisi, linatuuliza kwa mara nyingine tena kwa mshangao iwapo kuna mabadiliko katika miezi ya hivi karibuni, au kama bado tuko katika utandawazi wa kutojali. Na alionyesha kutambua, uwepo wa hatua nyingi ndogo ndogo za watu kujifunua kwa uwazi zaidi katika kuwapokea maskini hawa katika kituo acha Lampedusa. Na hivyo alitoa shukurani kwa wenyeji wa Lampedusa, akisema, kumekuwa na ishara ya ukarimu, hasa katika kuwajali wahamiaji wanao fika mbele ya macho yao, kusema, karibu “Wewe ni ndugu yangu. Ni Maelfu ya watu wanao kimbia vita, mapigano ya kikabila, mateso, umaskini na ukosefu wa matarajio ya baadaye.

Kardinali alieleza na kutoa wito kwa taifa la Italia kutochoka kuwapokea watu hawa wenye shida wanaotaka kuhamia Ulaya . Na aliomba mshikamano na jumuiya ya Kimataifa, usisinyae bali ukomae zaidi kupitia mashauriano, na uamushaji wa hisia za kuona aibu mbele ya miili ya watu wengi wanaokufa katika mapito magumu ya kutaka kuokoa maisha yao. Ingawa pia alionyesha kutambua kwamba, kuwasili kwa wageni wengi ni jambo la hatari linalopaswa kupatiwa jibu la kidharura katika kukabiliana na wimbi hilo. Lakini akahimiza kwamba, ni lazima kutoa jibu kupitia ubinadamu uliojenga katika amri ya kwanza ya Ukristo, Amri ya upendo kwa jirani. Na kwamba, kwa usimamizi na taratibu nzuri na salama, si tishio, lakini inaweza kujenga nafasi nzuri kwa bara la Ulaya, linalo onekana kuchoka, kupata hisia mpya za kufufua mizizi ya utamaduni wao.

Papa Francisco, wiki chache zilizopita, alikumbusha jinsi mizizi ya Kikristo ya Ulaya iliyo tambulika kwa ukarimu wake, barani, Afrika, sasa sifa hiyo njema na ya kuheshimiwa, inavyoyoyoma, katika harakati za utendaji wa manufaa ya umma. Kardinali alishauri, leo hii swali hili, Yu wapi ndugu yako, linapaswa kuwa sababu ya kugawana kwa usawa utajiri wa mali duniani, kama Papa alivyoeleza katika waraka wake wa Furaha ya Injili” Evangelii gaudium. ”








All the contents on this site are copyrighted ©.