Wananchi wa Nigeria wanaoishi Kaskazini mwa nchi hiyo ambao kwa miaka kadhaa wanakabiliana
na mashambulizi pamoja na vitendo vya utekaji nyara vinavyofanywa na Kikundi cha Boko
Haram, wameomba ulinzi kutoka Umoja wa Mataifa. Mjini Chibok, wanafunzi zaidi ya mia
mbili walitekwa nyara hadi sasa hawajulikani waliko.
Wananchi wanasema, Serikali
kuu imeshindwa kuwahakikishia wananchi wanaoishi Kaskazini mwa Nigeria ulinzi na usalama
ndio maana wanauomba Umoja wa Mataifa kuwasaidia kwa kuwapatia ulinzi na usalama dhidi
ya mashambulizi yanayofanywa na Kikundi cha kigaidi cha Boko Haram.
Takwimu
zinaonesha kwamba katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita watu zaidi ya mia mbili
wameuwawa kikatili kutokana na mashambulizi kumi na tano yaliyofanywa kwenye vijiji
kadhaa Kaskazini mwa Nigeria.