2014-07-05 13:32:06

Askofu mkuu Antonio Arcari ateuliwa kuwa Balozi Mpya wa Vatican Costa Ricca


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Antonio Arcari kua Balozi mpya wa Vatican nchini Costa Rica. Kabla ya uhamisho huu Askofu mkuu Arcari alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Msumbiji. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Arcari alizaliwa tarehe 8 Mei 1953 mjini Brescia, Italia.

Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa kunako tarehe 11 Juni 1977. Tarehe 18 Julai 2003 akateuliwa na Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Honduras. Tarehe 12 Desemba 2008 Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Msumbiji na sasa ameteuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Costa Rica.







All the contents on this site are copyrighted ©.