Majeshi Maalum (Special Forces) ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania yanayolinda amani
Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ni miongoni mwa vikosi bora 35
vya majeshi ya nchi mbali duniani vinavyokubali kuwa na ufanisi wa hali ya juu, uwezo
mkubwa wa kupigana na vilivyofundishwa vizuri. Kwa mujibu wa Mtandao wa Imgur Via
Distractify, Tanzania na jeshi lake ni nchi pekee ya Afrika kuweza kuwa na majeshi
yake miongoni mwa majeshi bora duniani.
Chini ya kichwa cha habari “35 Most
Badass Elite Fighting Units from Around the World” mwandishi, Micky Wren anaandika
kuwa hayo ndiyo majeshi bora duniani, yamefundishwa kwa kiwango cha juu kabisa, yana
silaha za kisasa kabisa, yameandaliwa vizuri kwa ajili ya operesheni ngumu za kijeshi
na yenye uwezo kukabiliana na adui katika mazingira yoyote kuanzia kumaliza uhuni
wa utekaji hadi kuwasambaratisha magaidi wenye uwezo mkubwa. Mwandishi anasema kuwa
orodha hiyo haikupangwa kwa mtitiriko wa uwezo wa kijeshi wa kila kikundi.
Vikosi
vilivyoko kwenye orodha hiyo ni kile cha Seal cha Jeshi la Maji la Marekani, SAS cha
Jeshi la Uingereza, Huntsmen Corps cha Majeshi Maalum ya Denmark, Majeshi Maalum ya
Ufaransa, Kikosi cha MARSOC, Majeshi Maalum ya Taiwan ambayo yanatumia kinga za usoni
zisizoweza kuingiliwa na risasi na Kikosi cha Irish Army Rangers cha Jamhuri ya Ireland.
Vingine
ni Gendarmerie cha Serbia, Kikosi Maalum cha Kukabiliana na Ugaidi cha JTF2 cha Canada,
Majeshi Maalum ya Uholanzi, Kikosi cha SBS, Majeshi Maalum ya Jamhuri ya Korea, Majeshi
Maalum ya Ufaransa, Majeshi Maalum ya Ubelgiji, Kikosi cha MJK cha Norway, Canadian
Joint Response Unit cha Canada, Majeshi Maalum ya Norway, Kikosi cha French Commando
Marine, Majeshi Maalum ya New Zealand, Kikosi cha Norwegian Armed Forces Special Command
na Kikosi cha Polish Grom cha Poland.
Vingine ni Kikosi cha US Army Special
Forces Sniper with Remington Modular Sniper Rifle, Majeshi Maalum ya Marekani, Majeshi
Maalum ya Indonesia, Majeshi Maalum ya Romania, Kikosi cha SASR cha Australia, Kikosi
cha KSK cha Ujerumani, Majeshi Maalum ya Ujerumani, Majeshi Maalum ya Israel – Shayetet
13, Majeshi Maalum ya Urusi – Spetsnaz, Majeshi Maalum ya Austria – Jagdkommando,
Majeshi Maalum ya Iraq, Majeshi Maalum ya Ujerumani ya SEK-M na Majeshi Maalum ya
Peru.
Wakati huo huo, Rais Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi ya leo, Alhamisi,
Julai 3, 2014, amemkaribisha Ikulu, Dar Es Salaam, Mwana wa Mfalme wa Japan, Akishino
pamoja na mkewe Malkia Akishono. Mwana Mfalme huyo ambaye anatembelea Tanzania, amewasili
Ikulu kiasi cha saa nne asubuhi na kufanya mazungumzo ya zaidi ya nusu saa na Mheshimiwa
Rais Kikwete.
Katika mazungumzo yao, Rais Kikwete amesema kuwa Japan ni mshirika
mkubwa na muhimu sana wa maendeleo ya Tanzania. “Tunathamini sana mchango wenu katika
maendeleo ya Tanzania na tunaendelea kuwashukuru sana. Ukizunguka nchini mwetu utaona
kwa macho yako miradi mingi na mikubwa ambayo imejengwa ama inajengwa kwa msaada wa
Japan.”
Rais kikwete ameongeza: “Pamoja na ushirikiano huu. Bado tunaamini
kuwa Japan inaweza kusaidia zaidi Tanzania hasa kwa kushawishi makampuni yake kuwekeza
katika sekta binafsi. Ukipita mitaa ya Dar es Salaam, magari tisa kati ya 10 ni ya
Kijapan. Ukiingia katika maduka ya vyombo vya elektroniki - televisheni, kompyuta,
camera, karibu kila kitu kinatoka Japan. Hali hii inathibitisha kuwa bidhaa vya Japan
zina soko kubwa na zinaweza kuzalishwa hata hapa nchini na makampuni binafsi.”
Rais
Kikwete pia ameitaka Japan kuangalia jinsi gani inavyoweza kusaidia ongezeko la watalii
kutoka Japan kuja kutembelea Tanzania kwa kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja
kutoka huko hadi Tanzania na nchi nyingine za Afrika. “Wataalii wengi kutoka Japan
wanashindwa kuja Afrika kwa sababu hakuna shirika hata moja la ndege la Japan ambalo
lina safari za kuja Afrika, hata Afrika Kusini hakuna.
Hii ndiyo maana hatuoni
watalii wengine kutoka nchi za kusini mashariki mwa Bara la Asia kutembelea vivutio
vyetu vya utalii,” amesema Rais Kikwete na kuongeza: “Kama kuna jambo halionekani
sasa katika uhusiano wa Tanzania na Japan ni uwekezaji katika sekta binafsi. Hili
ndilo jambo tunaloliomba.