2014-07-02 09:15:30

Mkutano wa Makardinali!


Baba Mtakatifu Francisko, Jumanne, tarehe 1 Julai 2014 alijumuika na Baraza la Makardinali wanane katika mkutano wao wa tano unaojadili marekebisho msingi katika Sekretarieti ya Vatican. Hili ni Baraza la Makardinali alilolichagua ili kumsaidia kutekeleza utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro kwa kuzingatia ushauri na maelekezo yaliyotolewa na Makardinali wakati wa mikutano yao elekezi.

Baba Mtakatifu Francisko pamoja na Makardinali wataendelea na mkutano wao hadi tarehe 4 Julai 2014. Itakumbukwa kwamba, Makardinali hawa waliwahi kufanya mikutano yao, tarehe 1- 3 Oktoba 2013; tarehe 3- 5 Desemba 2013; tarehe 17-19 Februari 2014.







All the contents on this site are copyrighted ©.