Askofu mkuu Bernadito C. Auza ateuliwa kuwa ni Mwakilishi wa kudumu wa Vatican Umoja
wa Mataifa
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Bernardito C. Auza aliyekuwa Balozi
wa Vatican nchini Haiti kuwa Mwakilishi Mpya wa kudumu wa Vatican kwenye Ofisi za
Umoja wa Mataifa zilizoko New York, Marekani.
Askofu mkuu Auza anachukua
nafasi ya Askofu mkuu Francis Chullikatt, aliyeteuliwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto
XVI kunako tarehe 7 Julai na kuanza kutekeleza utume wake kama Mwakilishi wa kudumu
wa Vatican kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa kunako tarehe 15 Septemba 2010.