2014-07-01 10:21:38

Heshumuni Mfungo wa Mwezi Mkutufu wa Ramadhani


Askofu mkuu Alfred Adewale Martins wa Jimbo kuu la Lagos, Nigeria katika ujumbe wa matashi mema kwa waamini wa dini ya Kiislam, katika kipindi hiki cha Mfungo Mtukufu wa Mwezi wa Ramadhani, anawaalika wanapofunga na kujinyima, wawakumbuke maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa Jamii.

Hiki ni kipindi ambacho wanaweza kufanya tafakari ya kina kuhusu upendo kwa Mungu na jirani pamoja na kukazia umuhimu wa watu kuishi katika msingi ya haki na amani, kwa kuheshimiana na kuthaminiana kama watoto wa Mwenyezi Mungu licha ya tofauti zao za kidini na kiimani.

Ni mwaliko kwa kushikamana na kusaidiana na watu wote wenye mapenzi mema kwa ajili ya ujenzi na ustawi wa maendeleo ya wananchi wa Nigeria; kwa kusimama kidete katika misingi ya haki na usawa hasa wakati huu Nigeria inapoendelea kuogelea katika mashambulizi ya kigaidi na ukosefu wa amani na usalama kwa watu wasiokuwa na hatia!

Askofu mkuu Martins anakichangamotisha Kikundi cha Boko Haram kuheshimu Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kuachana na vitendo na mashambulizi ya kigaidi.







All the contents on this site are copyrighted ©.