2014-06-30 16:15:09

Serikali na Kanisa vishirikiane kwa ajili ya mafao ya wengi!


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 30 Juni 2014 amekutana na kuzungumza na Mfalme Felipe VI na Malkia Letizia wa Hispania mjini Vatican, baadaye wamekutana na kuzungumza pia na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Monsinyo Antoine Camilleri, Katibu mkuu msaidizi wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Katika mazungumzo kati ya Baba Mtakatifu na wageni wake, Mfalme Felipe VI amesema hii ni safari yao ya kwanza nje ya Hispania kama mwendelezo wa safari kama hii iliyofanywa na Mfalme Juan Carlos I na Malkia Sofia kunako tarehe 28 Aprili 2014, kama sehemu ya mchakato unaopania kuimarisha ushirikiano kati ya Vatican na Hispania.

Katika mazungumzo yao, Baba Mtakatifu na mgeni wake wamegusia mambo mbali mbali, lakini zaidi umuhimu wa majadiliano na ushirikiano kati ya Kanisa na Serikali, kwa ajili ya mafao ya wananchi wote wa Hispania. Wamegusia pia matatizo yanayoendelea kujitokeza katika ngazi ya kikanda na kimataifa hasa katika maeneo ambayo mtutu wa bunduki unaendelea kutawala!







All the contents on this site are copyrighted ©.