2014-06-28 12:19:04

Watiwa mbaroni kwa kujihusisha na biashara haramu ya binadamu


Watu kadhaa wametiwa mbaroni nchini Niger, Afrika ya Kaskazini kwa kujihusisha na biashara haramu ya binadamu kutoka Nigeria. Hili ni kundi kubwa la watoto lililokuwa linauzwa kwa watu mbali mbali nchini Niger kwa kushirikiana na wanawake kutoka Nigeria, kadiri ya taarifa za Jeshi la Polisi la Niger.

Jeshi hili limefanya uchunguzi wa kina na kubaini kwamba, baadhi ya wanawake kutoka Nigeria walikuwa wanajihusisha na biashara haramu ya binadamu kutoka Nigeria. Hili ni kundi la wanawake wagumba ambao hawakubahatika kupata watoto, kumbe wanawategemea wanawake kutoka Nigeria kuwatafutia watoto kwa bei nafuu, lakini hatima yake, watoto hawa wanaishia kwenye mtandao wa biashara haramu ya binadamu.

Polisi imegundua kwamba, Benin nayo iko kwenye mkumbo wa biashara haramu ya binadamu. Jeshi la Polisi nchini Niger limewatia hatiani wanawake 18 na kati yao kuna wanawake wa "vigogo" Serikalini.All the contents on this site are copyrighted ©.