Hatimaye, baada ya kushikiliwa na kwa siku mbili na vyombo vya usalama kwenye Uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Khartoum Sudan, Meriam Yeya Ibrahim Ishag, mwanamke Mkristo
aliyekuwa amehukumiwa kucharazwa viboko na hatimaye adhabu ya kifo kwa kukana dini
ya Kiislam ameachiliwa huru tarehe 26 Juni 2014 na sasa anahifadhiwa katika eneo lenye
usalama zaidi, wakati jitihada za kumtafutia hati maalum za kusafiria zinaendelea
kufanywa.
Meriam Ishag mwenye watoto wawili ameolewa na Daniel Wani, kwa sasa
wana mpango wa kwenda kuishi nje ya Sudan na mipango ya kidiplomasia inaendelea ndani
na nje ya Sudan.