Ujumbe wa Kanisa la Kiorthodox kushiriki katika Siku kuu ya Watakatifu Petro na Paulo
miamba wa imani!
Katika Mapokeo ya maadhimisho ya Siku kuu ya Mtakatifu Petro na Paulo miamba wa imani,
ujumbe wa kiekumene kutoka Kanisa la Kiorthodox kwa mwaka huu 2014 utaongozwa na Askofu
mkuu Ioaniss Zizioulas, Makamu wa Rais Tume ya Pamoja ya Kimataifa ya Majadiliano
ya Kitaalimungu kuhusu Uekemene.
Tarehe 28 Juni 2014, ujumbe huu wa kiekumene
utakutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko na baadaye watazungumza pia na
viongozi waandamizi wa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Umoja wa Wakristo. Jumapili
asubuhi, wajumbe hawa watashiriki katika Ibada ya Misa Takatifu inayotarajiwa kuongozwa
na Baba Mtakatifu Francisko kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.
Itakumbukwa
kwamba, kila mwaka ifikapo tarehe 30 Novemba wakati wa maadhimisho ya Sherehe ya Mtakatifu
Andrea, Baba Mtakatifu hutuma ujumbe wa Kanisa Katoliki kushiriki katika sherehe hizi
huko Instanbull, kama mwendelezo wa majadiliano ya kiekumene miongoni mwa Wakristo.