2014-06-26 14:49:09

Kilimo na usalama wa chakula Barani Afrika


Kutokana na kiwango kilichofikiwa cha Tabia Nchi hivi sasa, nchi za Afrika hazina budi kuungana na kuchukua hatua za kupunguza madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa kwa pamoja. Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo tarehe 25 Juni, 2014 Mjini Malabo, Equatorial Guinea wakati akifungua Mkutano wa Wakuu wa Nchi 11 zinazounda Kamati ya Mazingira ya Nchi za Umoja wa Afrika.


"Suala la Tabia Nchi baranil Afrika ni changamoto na fursa pia kwani kama tukifanya uamuzi mzuri tunaweza kupata manufaa kutokana na mbinu mbalimbali zilizopo za kupunguza madhara yake".


Rais Kikwete amesema na kuzitaka nchi kulichukulia suala la Tabia Nchi kwa umakini mkubwa kwani kwa hali tuliyofikia hivi sasa, hakuna chaguo lingine bali kuangalia njia za kupunguza athari zake tu. Nchi wanachama wa Kamati ya Mazingira ya AU in Tanzania ambaye ndiye Mwenyekiti, Algeria, Ethiopia, Congo-Brazaville, Kenya, Mauritania, Mauritius, Msumbiji na Uganda.


Kamati ya Mazingira ya AU ina jukumu la kuongoza nchi za Afrika katika kupanga mikakati, mbinu na njia mbalimbali za kukabiliana na madhara ya Tabia Nchi barani Agrola na pia kuzitumia changamoto zake katika kuleta maendeleo na matokeo chanya katika jitihada hizo kwa manufaa ya nchi za Afrika.


Kamati ya AU imesisistiza kuwa nchi za Afrika zinahitaji kuboresha uwezo wake wa kupata taarifa za tahadhari katika ngazi zote, uwezo wa kifedha, mawasiliano na usafirishaji katika miji yake na pia kuongeza uwezo wake wa kuzuia mafuriko kwa kutumia njia za kisasa, uwezo wa kupanga miji na kupunguza athari za sasa na baadaye kwa ajili ya wananchi wake na uchumi pia. Amesema pia bara la Afrika linahitaji elimu na maarifa zaidi kwa wananchi wake kwa ujumla kuhusu athari hizi na tahadhari kwa ujumla.


Rais amesema pamoja na kwamba nchi za Afrika zinachangia asilimia ndogo katika suala la Tabia Nchi, Afrika haina budi kuzitaka nchi zinazoendelea kuchangia zaidi katika mahitaji na juhudi mbalimbali za bara la Afrika katika jitihada zake za kupambana na athari za Tabia Nchi. Rais Kikwete yuko Malabo kuhudhuria kikao cha siku mbili I cha Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (AU) kinachoanza tarehe 26 Juni 2014 na kumalizika tarehe 27 Juni,2014. Ajenda ya kikao cha Mwaka huu ni Kilimo na Usalama wa Chakula Barani Afrika.
All the contents on this site are copyrighted ©.