2014-06-26 16:01:38

Familia ni kito tha thamani!


Hati ya kutendea kazi kwa ajili ya Sinodi maalum ya Maaskofu kwa familia imezinduliwa mjini Vatican kwa kuongozwa na kauli mbiu "Changamoto za kichungaji kwa familia mintarafu Uinjilishaji Mpya". Sehemu ya kwanza inawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kutangaza Injili ya Familia kwa watu wa nyakati hizi.

Sehemu ya pili ya hati hii inawataka waamini kuangalia mikakati ya shughuli za kichungaji kama njia ya kupambana na changamoto mpya katika familia. Sehemu ya tatu ni mwaliko kwa Familia ya Mungu kuwa wazi katika kupokea zawadi ya maisha na kuwajibika katika malezi.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anasema kwamba, familia ni kito cha thamani kwa maendeleo ya mwanadamu na jamii katika ujumla wake!All the contents on this site are copyrighted ©.