Mapema Jumatano hii kabla ya Katekesi yake, Papa Francisko alikwenda katika ukumbi
Paulo V1, wa mjini Vatican, kusalimia mahujaji na wageni wagonjwa, walikuwa wamekusanyika
katika ukumbi huo, pia kwa lengo la kusikiliza Katekesi ya Papa. Akisalimiana
nao, Papa aliwafariji wagonjwa akisema , "muda si mrefu nitakwenda katika uwanja
wa Kanisa Kuu, kukutana na umati mkubwa wa watu, mahali penye joto kali, na pia
kuna hatari ya mvua kunyesha , hivyo si mahali panapofaa kwa mtu mgonjwa". Hivyo Papa
aliwasihi wafuatile Katekesi yake wakiwa katika ukumbi huo kupitia screeni kubwa,
iliyowekwa mbele yao. Na kwa pamoja na wagonjwa hao, walitolea sala kwa Mama Yetu
Maria na kuomba baraka za Mwenyezi Mungu . Papa aliwasihi wasimsahau katika sala
zao. “ Asante sana”, alimalizia.