2014-06-25 11:04:42

Kampeni ya kudhibiti vifo miongoni mwa watoto na wajawazito!


Wananchi wanaoishi katika kitongoji cha Isiolo, nchini Kenya, ambao wengi wao wanajishughulisha na shughuli za kilimo, wanakabiliwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na matumizi ya maji yasiyo safi wala salama pamoja na mazingira yao kukithiri kwa uchafu. Mambo haya yanachangia kwa kiasi kikubwa vifo vya watoto wadogo na wanawake wajawazito.

Kutokana na changamoto hizi, Kamati ya Ushirikiano wa Madaktari, CMM kwa kushirikiana na Chama cha Watu wa kujitolea kimataifa pamoja na viongozi mahalia, wameanzisha kampeni ya kuhamasisha matumizi ya maji safi na salama pamoja na utunzaji bora wa mazingira kama njia ya kupambana na magonjwa ambayo yanaweza kuzuilika na kutibika kwa urahisi.

Kampeni hii inalenga pia kuvihusisha vituo Vituo vya Afya na Zahanati zilizoko wilayani Gambella, ili kufanikisha kampeni hii.







All the contents on this site are copyrighted ©.