Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu 23 Juni 2014 amekutana na kuzungumza na Askofu
mkuu Ricardo Blazquez Peres, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Hispania pamoja na
ujumbe wake kwa kuwataka waendelee kujielekeza zaidi katika kuhamasisha maisha na
utume wa shughuli za kimissionari ndani ya Kanisa.
Viongozi wa Baraza la Maaskofu
Katoliki Hispania, wamemwonesha Baba Mtakatifu mikakati na shughuli za kichungaji
zinazotekelezwa na Kanisa Katoliki nchini Hispania. Mkazo ni kwa ajili ya kumhudumia
mwanadamu: kiroho na kimwili, lakini kwa kutoa kipaumbele cha kwanza kwa maskini na
wote wanaosukumiziwa pembezoni mwa Jamii.
Baba Mtakatifu amekutana na uongozi
wa Baraza la Maaskofu Katoliki Hispania, uliochaguliwa hivi karibuni. Viongozi wa
Baraza la Maaskofu Katoliki Hispania, wamekutana na kuzungumza pia na viongozi waandamizi
kutoka Sekretarieti ya Vatican.