2014-06-24 09:07:23

Sr. Kapuli auwawa kikatili kwa kupigwa risasi kifuani Dar es Salaam!


Sr. Crescentia Kapuli (52) wa Shirika la Bikira Maria Malkia wa Mitume, Jimbo Katoliki la Mbeya meuwawa kikatili kwa kupigwa risasi kifuani na watu wanaosadikiwa kuwa ni amajambazi, siku ya Jumatatu alasiri, tarehe 23 Juni 2014 wakati akitoka Benki, eneo la Ubungo Riverside, Dar es Salaam.

Habari hizi zimethibitishwa na Camillus Wambura Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kindondoni. Katika tukio hili, Dreva Mark Mwarabu naye amejeruhiwa kwa risasi na anaendelea kupatiwa matibabu na Polisi inaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hili.

Jimbo kuu la Dar es Salaam Alhamisi tarehe 26 Juni 2014, majira ya saa 5:00 asubuhi linatarajia kuadhimisha Ibada ya Misa takatifu kwenye Parokia ya Mtakatifu Gaudencia, Makoka kwa ajili ya kumwombea na hatimaye, kuanza safari kuelekea Jimboni Mbeya, atakapopumzishwa kwenye makao ya milele pamoja na watawa wenzake.

Marehemu Sr. Crescentia Kapuli alikuwa ni mhasibu wa Shule ya Sekondari na Chuo cha Ufundi cha Mwenyeheri Anwarite, Makoka na kwamba, mauti yamemfika wakati akitelekeza utume wake. Kabla ya kuhamishiwa Jimbo kuu la Dar es Saalam, shuleni hapo aliwahi pia kuwa Mhasibu wa Jimbo Katoliki Mbeya. Familia ya Mungu nchini Tanzania na kwa namna ya pekee watawa wenzake wameshikwa na simanzi kubwa kuona baadhi ya watu wenye uchu wa mali wakikaatisha maisha ya Sr. Crescentia Kapuli. RIP.







All the contents on this site are copyrighted ©.