2014-06-23 09:41:40

Ekaristi ni ishara ya upendo wa Mungu usio na kipimo, na kutesa wengine ni dhambi ya mauti asema Papa


Ekaristi Takatifu daima hutuonyesha kwamba,hakuna kipimo katika upendo wa Mungu. Ni maelezo ya Papa Francisko, Jumapili mchana, wakati akisalimia maelfu ya mahujaji na wageni tokea dirisha la chumba chake cha kujisome. Umati wa watu waliokusanyika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kwa ajili ya sala ya Malaika wa Bwana.

Hotuba fupi ya Papa, ilitafakari juu ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Mwili wa Bwana, iliyoadhimisha katika Makanisa Katoliki yote duniani , siku ya Jumapili. Umati huo wa Watu ulishangilia kwa nguvu wakati Papa alipokemea na kulaani mateso dhidi ya wengine , kwamba kutesa wengine ni dhambi kubwa, ni dhambi ya mauti. Alieleza kwa kuwakumbuka waathirika wa mateso, ambao watakuwa hoja rejea wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa tarehe 26 Juni.

Alisema, Mwili “uliovunjwa " kwa ajili ya wengine, Mwili wa Bwana , “Corpus Domini, Mwili wa Kristo, ubinadamu hautoi "kitu" isipokuwa kutolea "nafsi", unakuwa ni wito wa kweli wa Mkristo, katika kuhudumia wengine, ambao chimbuko lake ni Ekaristi. Na usharika na Mwili wa Yesu, Papa Francis,alisistiza, huleta mabadiliko makubwa, katika kuiga maisha ya Yesu, mkate wa mwili uliovunjwa kwa ajili yetu sisi, unao tuonyesha tabia ukarimu kwa wengine, kuwa na tabia ya majitoleo ya maisha kwa ajili ya wengine.
Papa Francisko aliendelea kueleza kwamba, kila wakati tunapo shiriki katika Misa na kulishwa kwa Mwili wa Kristo, mbele ya Yesu na Roho Mtakatifu, hufanya kazi ndani yetu, maumbo moyo wetu yanapaswa kubadilika katika mitazamo ya ndani katika tafsiri ya tabia kulingana na Injili. Kwanza, ni usikivu kwa neno la Mungu, kisha udugu kati yetu, na ujasiri wa ushuhuda wa Kikristo, unaoshamiri kwa upendo, uwezo wa kutoa tumaini kwa matumaini, kukubali kukataliwa. Huu ndiyo mtindo wa Maisha ya Kikristo yaliyo komaa. Ekaristi, hulisha moyo wenye njaa , ni chakula kinacho tia ndani ya mioyo yetu uwezo wa kupenda, si kwa kipimo cha binadamu , ambayo daima huwa na mipaka , lakini kulingana na kipimo cha Mungu.

Papa alifafanua na kusisitiza , ndiyo tunasema kipimo cha Mungu , lakini Mungu hana kipimo. Upendo wake mkubwa mno kiasi kwamba hauna kipimo, si kwa marefu au mapana au kina . Huwezi kupima upendo wa Mungu maana hauna kipimo! Na hivyo ndivyo tunavyotakiwa sisi kuwa na uwezo wa kuwapenda watu wote bila kipimo hata wale ambao tunaona wazi hawana upendo kwetu. Papa alionyesha kutambua kwamba hili si jambo jepesi, kumpenda asiyekupenda lakini ndivyo inavyotakiwa . Na kwamba , twafahamu kwamba, mtu huyu hataki kushirikiana nasi au kuwa mmoja wetu kwa sababu atuchukia, sisi pia hupoteza hamu ya kumpenda mtu huyo. Lakini Neno la mungu lasema ni lazima kuwapenda watu hao. Ni kuwapenda hata wale ambao hawana upendo kwetu. "

Papa anasema,” Mkate wa upendo ulivunjwa, ili kuonyesha utendaji wa kinyume, ubaya kwa wema, chuki kwa kusamehe na utengano kuwa umoja. Ni kuigundua furaha ya kweli, ngao ya kukabiliana na changamoto ,ni kupokea kama zawadi kubwa ya kwanza katika maisha, tuliyo pewa bila kustahili.

Ni Mwili uliovunjwa kwa upendo kwa ajili ya kila mtu anayekabiliana na vurugu za kutisha za binadamu. Papa aliongeza baada ya sala ya Malaika wa Bwana, akiwakumbuka waathirika wa mateso, na Maadhimisho yajayo ya Siku ya Umoja wa Mataifa, hapo Alhamisi Siku Juni 26. Katika mazingira hayo, Papa alikemea vikali kila aina ya mateso na kuwaalika Wakristo wote washiriki vyema katika kila juhudi zinazo tafuta kutokomeza ukatili na mateso kwa binadamu. Kutesa watu ni dhambi ya mauti! dhambi kubwa sana.








All the contents on this site are copyrighted ©.