2014-06-16 07:41:44

Jumuiya ya Wayahudi Roma inamwalika Papa kutembelea Sinagogi lao!


Bwana Riccardo Pacifici, Rais wa Jumuiya ya Wayahudi wanaoishi mjini Roma, Jumapili jioni ameongoza ujumbe wa Wayahudi kutoka Roma uliokuwa unahudhuria mkutano kati ya Baba Mtakatifu Francisko na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, umetoa mwaliko rasmi kwa Baba Mtakatifu Francisko kutembelea Sinagogi lao. Mwaliko huu umepokelewa na Baba Mtakatifu kama sehemu ya mwendelezo wa urafiki kati ya waamini wa dini mbali mbali.

Itakumbukwa kwamba, kunako mwaka 1986 Mtakatifu Yohane Paulo II alitembelea Sinagogi hili na baadaye kunako mwaka 2009 Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI alitembelea tena.All the contents on this site are copyrighted ©.