2014-06-14 14:40:18

Ratiba elekezi kwa Mwezi Julai- Agosti 2014


Taarifa kuhusu shughuli mbali mbali zinazotarajiwa kutendwa na Baba Mtakatifu Francisko inaonesha kwamba, kwa mwezi Julai hakutakuwepo na Katekesi zake zinazotolewa kila Siku ya Jumatano. Ni Kipindi cha mapumziko kwa Baba Mtakatifu Francisko. Katekesi zake zitaanza tena tarehe 6 Agosti, 2014, Siku kuu ya kung'ara Bwana.

Tarehe 13 Agosti, hakutakuwa na Katekesi kwani Baba Mtakatifu atakuwa njiani kuelekea Korea katika maadhimisho ya siku ya sita ya vijana Barani Asia inayoongozwa na kauli mbiu "Ondoka, uangaze, kwa kuwa nuru yako imekuja, na utukufu wa Bwana umekuzukia". Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kurejea tena mjini Vatican tarehe 18 Agosti 2014. Katekesi itaanza tena hapo tarehe 20 na 27 Agosti 2014.

Baba Mtakatifu Francisko ataendelea kusali na kutafakari na waamini wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana katika kipindi cha Mwezi Julai na Agosti, isipokuwa Jumapili zile ambazo atakuwa safarini nchini Korea ya Kusini. Wakati wa likizo ya kipindi cha kiangazi, Ibada za Misa Takatifu kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Martha mjini Vatican zimesitishwa na zitaanza tena mwanzoni mwa Mwezi Septemba 2014.All the contents on this site are copyrighted ©.