2014-06-14 10:19:42

Papa Francisko azungumzia kipindi cha Papa Pius XII na Utengano Ulaya..


(Vatican Radio) Baba Mtakatifu Francisko , ametetea kwa nguvu nyaraka zilizoandikwa juu ya utendaji wa Papa Pius XII , akisema, anajali ukosoaji wote unaotolewa kwa Papa Pius XII, wakati wa harakati za utengano barani Ulaya. Papa Francisko alieleza katika mahojiano na gazeti la La Vanguardia, gazeti mashuhuri katika mji wa Barcelona.

Papa Francis alionyesha kujali lawama zote zile zinazo tolewa kwa Mtumishi wa Mungu , Mnyenyekevu Papa Pius XII, bila ya kuona jinsi alivyojitahidi kukoa maisha ya Wayahudi, waliokua wamefichama kisiri katika nyumba za watawa za Roma na miji mingine ya Italia, kama vile makazi ya majira ya Kipapa ya Castel Gadolfo, kusalimisha maisha yao dhidi ya udhalimu w utawala wa Nazi.

Alisema, hana maana ya kusema kwamba Papa PiusXXII, kama binadamu hakufanya makosa, hakuna binadamu anayeishi kama malaika bila makosa. Papa Francisko anasema , hata yeye mwenyewe anakiri kwamba kuna wakati anakosea, hili ni jambo la kawaida kwa binadamu. Lakini pia binadamu huyu hakosi kuwa na mazuri anayoyafanya. Na hivyo ni vyema, wakati wa kulalamika pia kutaja mazuri yaliyofanywa na Papa Pius XII, kwa mtazamo wa mazingira ya vita na upinzani mkubwa wakati wake.

Aliongeza kuwa yeye hushikwa na simanzi, anaposikia watu wakikosoa dhidi ya Papa Pius XXII na Kanisa ilivyo kuwa wakati wa Vita Kuu ya 2, na kupuuza uhalifu uliofanywa na Mamlaka za kiserikali na majeshi yake. Papa Francisko ,aliongeza, pamoja na wapinzani wa Nazi kuujua kikamilifu mtandao wa reli iliyotumiwa na jeshi la Nazi kuwachukua Wayahudi hadi kwenye kambi za mateso, mbona majeshi pinzani hayakushambulia reli hizo ? Walikuwa picha, "alisema, lakini hawakubomu njia hizi za reli. Kwa nini? Papa alihoji na kuwataka wanaolalamika pia kufanya uchunguzi wa kina juu kwa mambo yote na kuwa wakweli.
Alipoulizwa kuhusu hali eneo la Catalonia nchini Hispania linalotaka kujitenga, alisema yeye hujali migawanyiko yote. Na alitaja tofauti iliyopo kati ya "uhuru wa ukombozi" na "uhuru kwa migawanyiko, kwa kutoa mfano wa Yugoslavia ya zamani ambapo kuna watu wa tamaduni nyingi tofauti na hakuna kinachowaunganisha.

Na kwa hali katika Catalonia, pia Kaskazini mwa Italia, na Scotland, Papa Francis alisema kila sehemu inapaswa kuzama katika kuona misingi ya madai yake kwa kina, kwa ajili ya kupata ukweli katika madai hayo , ili lisiwe ni jambo la kupapukia tu au wachache kulazimisha kujitenga kwa sababu zao binafsi. Ni suala ambalo ni lazima kutazamwa kwa kibano," alisema.

Papa pia aligeukia masuala ya kiuchumi, akisema, ni jambo la kukasirisha kuwa baadhi ya nchi kuwa na kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana zaidi ya 50%, mamilioni ya vijana wa Ulaya hawana kazi.Na alionya dhidi ya watu wazima kukiondoa kizazi kizima cha vijana katika mfumo wa ajira kwa lengo la kudumisha mfumo wa uchumi ambayo haufanyi kazi tena , mfumo ambao ili mtu aweze kuishi ni lazima apambane, kama ambavyo hufanya himaya kubwa, lazima kupambana daima , aliliambia gazeti la Catalonia.

Papa ameasa dunia haiwezi tena kupigana Vita Kuu ya III, na kisha kuwa na vita vya kimikoa kwa maana ya kutaka kutengeneza na kuuza silaha.?" Aliendelea kusema, uwepo wa mizania ya uchumi ashiki, nchi zenye uchumi mkubwa dunia humtoa mtu maskini sadaka katika miguu ya nguvu ya fedha, iliyosafishika. .

Papa Francis pia alizungumza juu ya maisha yake kama Papa, kwamba kwake yeye huduma kama mchungaji ni muhimu zaidi ya mwelekeo wote katika wito wake. Na akieleza kama ana hofu juu ya maisha yake alisema, hutembea na gari dogo la Kipapa lenye kuwa na vioo visivyo penyeka risasi, kama ukuta kati yake na watu, kwa kuwa ni kweli kwamba chochote kibaya kinaweza kutokea, lakini akasema pia hata hivyo katika umri wake hana mengi ya kupoteza," alisema.

Aidha alizungumzia kustaafu ya Papa Benedict XVI kwamba ilikuwa "ishara kubwa" ambayo ilifungua mlango wa kuundwa kwa taasisi ya baadaye ya Mapapa wastaafu. Alifafanua , kutokana na kiwango cha umri wa kuishi kuongezeka kwa wakati huu, inakuwa si busara kuendelea kubaki madarakani katika umri mkubwa maana si rahisi kuendelea na utendaji wa haraka kama inavyotakiwa. Pia yeye atafanya hivyo kama ikibidi, na hivyo anamwomba Bwana amuangazie wakati huo ukiwadia, amwambie kile kinachofaa kufanya na kwa hakika atamwambia.

Na pia bila maelezo mengi ,aliahidi kwamba atakuwa karibu na raia wa Brazil, na kuwataka kutoegemea upande wowote wakati huu wa Kombe la Dunia. Na alikataa kujibu swali ni nani hasa anapendelea ashinde katika mashindano haya.


Gazeti lilihitimisha mahojiano kwa kumwuliza Baba Mtakatifu jinsi angependa kukumbukwa kihistoria. Papa alijibu hana wazo juu ya hili, lakini hatimaye alisema, lakini hufurahia kusikia mtu akikumbukwa kwa kutajwa, alikuwa mtu mwema , alijitahidi kufanya mengi mazuri au hakuwa mbaya kiasi hicho, maelezo kama hayo humfurahisha.








All the contents on this site are copyrighted ©.