2014-06-14 12:32:18

Gusweni na mateso ya wananchi wa Syria!


Wananchi wasiokuwa na hatia nchini Syria wanaendelea kupoteza maisha yao kutokana na vita pamoja na mashambulizi ya kigaidi na kwa sasa inaonekana kwamba jitihada za kidiplomasia za kutafuta haki, amani na utulivu nchini Syria zinaonekana kugonga mwamba!

Jumuiya ya Kimtaifa bado imegawanyika na inashindwa kuchukua hatua madhubuti ili kukomesha vita hii ambayo imeendelea kusababisha majanga makubwa kwa wananchi wengi wa Syria. Hapa majeshi ya Serikali na wapinzani yanaendelea kupambana usiku na mchana na kwamba, hata wapinzani wamegawanyika tena wao kwa wao!

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anasema kwamba, kuna hatari ya kusahau mateso na mahangaiko ya watu ambao hawawagusi kwa karibu. Kuna haja ya kutenda na kuendelea kusali kwa ajili ya kuombea amani na utulivu nchini Syria.All the contents on this site are copyrighted ©.