2014-06-13 15:36:08

Daima Mungu ni msaada kwa watumishi wake - Papa


(Vatican Radio) Bwana kabla ya kutupa dhamana ya kumtumikia , kwanza hutuandaa ili tuweze kufanya vizuri. Na mwitikio wetu ni lazim uwe katika misingi ya sala na uaminifu. Papa amesisitiza katika hotuba yake wakati wa Ibada ya Misa ya asubuhi Ijumaa hii kaika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta.

Papa alieleza juu ya ujasiri na udhaifu wa binadamu akisema inaweza kutokea, kwa mpizani jasiri wa ibada ya sanamu katika huduma ya Mungu, siku moja akasononeka nakukata tamaa hadi kutamani kifo, kwa sababu tu ya kitisho cha mtu mmoja. Katika majaribu haya, tuna huzunika na poteza matumaini hata kutamani kufa kwa sababu tu tumepata upinzani, katika kutimiza utume wetu, mtu mmoja ametutisha. Lakini hakuna sababu za kukata tamaa bali ni kusimama imara katika utambuzi kwamba, daima ni k azi ya Mungu, kusawazisha hali hizi mbili ujasiri na udhaifu wa binadamu, siku zote tunapokuwa aminifu kwake.
Papa alieleza na kurejea maelezo juu ya Nabii Eliya kama ilivyoandikwa katika kitabu cha kwanza cha Wafalme. Katika hotuba yake, Papa Francis alichukua maelezo haya kuwa ni mfano wa uzoefu wa kila mtu wa imani.

Alisema, wakati Bwana anataka kutupatia ujumbe, anataka kutupatia kazi, na ni Yeye anayetuandaa sisi kuwa tayari. Anatuandaa kuitenda kazi yake vizuri kama alivyo mwandaa Eliya. Na jambo la muhimu katika hili si tu kukutana na Bwana, la hiyo haitoshi. Kilicho muhimu zaidi ni kuishika njia yake na kutembea humo hadi mwisho wa utume alio tudhaminisha Bwana . Na hii ndiyo tofauti kati ya kazi za kitume tunazokabidhiwa na Bwana, na kazi zetu za kawaida. Kukamilisha kazi yake, ni wajibu tena kwa uaminifu na vizuri ...
Papa alikamilisha kwa kumeomba Bwana atupe neema ya kuturuhusu kujiandaa vyema kila siku katika njia ya maisha yetu, kwa ajili ya kuwa mashahidi wa wokovu wa ulio letwa na Yesu. "








All the contents on this site are copyrighted ©.