Papa aonya hakuna furaha ya kweli katika rushwa na ufisadi ..
Papa Francisko ameasa kwamba, ndani ya maisha ya kupenda kudhulumu wengine kwa rushwa,
ufisadi, au biashara na kazi zinazokiuka utu mtu , na kumkana Mungu, maisha hayo
hayana furaha ya kweli. Licha ya utajiri wa fedha na vitu wanavyoweza kujikusanyia,
ndani ya mioyo yao hawana furaha. Moyoni wamejaa wasiwasi na mashaka.
Baba
Mtakatifu Francisko , alionya siku ya Jumatano, wakati akitoa Katekesi kwa mahujaji
juu ya vipaji vya Roho Mtakatifu. Katika katekesi hii, ambayo ilikamilisha mfululizo
wa mafundisho ya Papa Francisko juu ya vipaji saba vya Roho Mtakatifu, Papa alizungumzia,
kipaji cha kumcha Mungu. Alisema kumcha Mungu , haina maana ya kuwa mwoga, lakini
ni kuwa wanyenyekevu na watiifu mbele ya uso wake kama vile mtoto kwa baba yake. Na
kwamba sote twapaswa kufahamu kwamba , siku moja tutapaswa kutoa hesabu ya utendaji
wetu Mbele yake.
Papa aliendelea kufafanua kwamba, Mungu hutupokea sisi kwa
upendo mkuu. Na hivyo nasi tunatakiwa kufanya mengi mazuri kwa wengine. Lakini inahitaji
kuishinda roho ya dhambi inayotuweka mbali na Mungu. Roho Mtakatifu daima yu karibu
nasi kusaidia kufanya mabadiliko ya moyo na kuzungumza na Baba, Mungu wetu.
Papa
alieleza na kuwataja mafisadi na wapenda rushwa kwamba , kwa nje wanaweza huonekana
kuwa na furaha lakini ndani ya mioyo hao hawana amani, kwa kuwa matunda yote ya rushwa,
huipotosha roho, na hukosesha ujasiri wa kwenda kwa Baba Mungu, ambaye huonekana
ndani ya kuwapenda wengine.
Aidha Papa alitaja, mtu anayeishi maisha ya kudhulumu
wengine na kumkana Mungu, mtu huyo hawezi kuwa na furaha, maana moyo wake uko
mbali na upendo na faraja za Mungu Baba! Na aliangalisha katika matunda ya rushwa
, na wale ambao wanaishi kwa mapato ya biashara ya binadamu au kwa nguvu kazi ya
watumwa akisema kwamba , hata kama wanapata fedha za kutosha ndani mwao hawana furaha
kamili!
Watu hawa mara nyingi hawamchi Mungu, au hujionyesha kwa nje wako
karibu na Mungu lakini vitendo vy viko kinyume na mapenzi ya Mungu, hivyo wako mbali
na Mungu . Papa alieleza na kutoa mfano wa wale wanao tengeneza silaha kwa lengo la
kuchochea vita .. au watu ambao wanasema hawana haja ya kusikia Neno la Mungu, wanaoona
wamejitosheleza wenyewe na badala yake wanazalisha vifo, wote hao hawamchi Mungu
, ndiyo maana wanafanya biashara hizi za kifo. Kumcha Mungu, hutufanya kuelewa kuwa
siku moja, tutatakiwa kutoa hesabu ya vitendo vyetu kwa Mungu.