2014-06-11 11:25:31

Papa apeleka salaam za Rambirambi kufuatia kifo cha Kardinali Bernard Agre


Jumanne mara baada ya kupewa taarifa ya kifo cha Kardinali Bernard Agre, Baba Mtakatifu Francisko alipeleka salaam za rambirambi kwa Kardinali Jean Pierre Kutwa ,wa Jimbo Kuu la Abidjan, aliyechukua nafasi ya mstaafu Askofu Mkuu Agre.
Katika salaam hizo zilizotumwa kwa njia ya Telgramme na Katibu wa Vatican , Kardinali Pietro Parolin, Papa Francisko, ameonyesha huzuni yake kwa kuondokewa na mpendwa Kardinali Bernard Agre, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 88, akiwa mjini Paris, ambako alikwenda kwa ajili ya matibabu. Papa amemkumbuka Marehemu , kwamba, alikuwa ni mtu Mungu, aliyependa bila ya akujibakiza kuitangaza Injili na kumwendeleza binadamu kiroho na kihali .
Papa ameendelea kusema, wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mtumishi hodari wa Mungu , angependa kutoa salaam zake za faraja na baraka za kitume kwa Maaskofu wote, Mapadre wa Jimbo Kuu la Abdjan, , familia ya Marehemu na marafiki zake, na kwa wale wote watakaoshiriki katika Ibada za msiba huu na maziko.
Kwa kifo cha Kardinali Bernard Agre, , Chuo cha Makardinali kimebaki na jumla ya Makardinali 213 Makardinali, 118 ni wapiga kura na 95 si wapiga kura, kwa mujibu wa sheria ya “Conclave”. Tunamwombea Pumziko la amani.








All the contents on this site are copyrighted ©.