2014-06-11 12:38:40

Papa afafanua maana ya Kumcha Mungu


Baba Mtakatifu Francisko, amehitimisha mfululizo wa mafundisho yake juu ya tuzo saba za Roho Mtakatifu, akiizungumzia maana ya uchaji kwa Mungu kwamba, haina maana ya kumhofia Mungu, maana twajua kwamba Mungu ni Baba anayetupenda. Alitoa wokovu kwetu, na daima husamehe. Kwa hiyo, hakuna sababu ya kuwa na hofu juu yake! Hata hivyo, ni zawadi ya Roho, ambaye hutukumbusha jinsi sisi tulivyo wadogo mbele ya Mungu na upendo wake, na kwamba ni vyema kwetu, kujikabidhi kwa Mungu kwa unyenyekevu, heshima na uaminifu, katika mikono yake. Huo ndiyo uchaji wa kweli kwa Mungu: kujiweka katika wema wa Baba yetu ambaye anatupenda sisi sote sana!

Katekesi hii ya Papa, iliyotolewa chini ya vifungu vitatu, ilianza na tafakari juu ya Roho Mtakatifu,anapokuja na kukaa katika mioyo yetu, na kuwa chemichemi ya faraja na amani, na kutuongoza katika kujisikia kama sisi ni wadogo , kama ilivyoelezwa na Yesu katika mafundisho yake, kuyaweka matumaini, hisia na utendaji na ulinzi wote kwa Mungu , kama vile mtoto kwa baba yake! Na hizi ndizo hisia , ambamo Roho Mtakatifu hufanya kazi yake katika mioyo yetu, kutufanya kujisikia kama watoto katika mikono ya Baba yetu. Kwa maana hii, basi, na tuwe na uelewa chanya katika kumcha Mungu, kwamba ni kuwa wanyenyekevu, na watu wa shukrani na sifa, zenye kujaza mioyo yetu na matumaini. Mara nyingi, kwa kweli, tunashindwa kuelewa mpango wa Mungu, na kutambua kwamba hatuwezi kuwa na uhakika wa kufurahia wenyewe furaha na uzima wa milele. Ni katika uzoefu wa mipaka ya uwezo wetu na umaskini wetu, ingawa, kwamba, Roho Mtakatifu hutufariji na kutufanya kujisikia kuwa muhimu iwapo tu tunakubali kuongozwa na Yesu katika mikono ya Baba yake.

Na hiyo ndiyo sababu kwamba , tunahitaji sana zawadi ya Roho Mtakatifu. Papa aliendelea kufundisha katika kipengere cha pili kwamba, kumcha Mungu , hutufanya na kutupa utambuzi kwamba, kila kitu huja kwa njia ya neema na kwamba nguvu yetu ya kweli ipo tu katika kufuatana na Bwana Yesu na katika kujiweka kwa i Baba, ili aweze kufanya yote upya kwa wema wake na rehema yake. Papa alieleza na kuwahimiza waamini kuifungua mioyo yao, kwa ajili ya wema na huruma ya Mungu inayo kuja kwetu. Roho Mtakatifu na zawadi ya uchaji kwa Mungu, ndiyo inayofungua mioyo. Kuufungua moyo kwa sababu ya msamaha, huruma, wema, na faraja kutoka kwa Baba huja kwetu. Kwa sababu sisi ni watoto wapendwa wa Baba.

Katika kipengere cha tatu, Papa ameizungumzia maana ya kumcha Mungu kuwa ni kumfuata Bwana kwa unyenyekevu, usikivu na utii. Ni kuwa na mtazamo katika matumaini , bila kukata tamaa, hata kama inaonekana kuwa ni taratibu mno, lakini kwa ajabu na furaha, furaha ya mtoto anayetambua kuwa anapendwa na Baba. Kumcha Mungu, kwa hiyo, haina maana ya kuonea aibu Ukristu , bali ni utiifu, wenye kuzaa ujasiri na nguvu! Ni zawadi ambayo huwafanya waamini Wakristo, kuwa na shauku, isiyokoma katika kumcha wana kwa utii na huku wakiongozwa na Urafiki na upendo wake! Ni kuwa mshindi kwa upendo wa Mungu: na hii ni jambo Jema. Papa ameeleza na kumtaka kila mmoja kujenga mwenyewe Urafiki na upendo wa Baba, anayetupenda kwa moyo wake wote. Lakini ni muhimu kuwa makini kutoichafua zawadi hii ya Roho Mtakatifu kwa ukaidi wa dhambi. Papa alieleza na kutaja hali za ukana Mungu, mapenzi kwa fedha na mali, ubatili na kiburi cha kutomfia Mungu.

Aidha Papa alitaja, mtu anayeishi maisha ya kudhulumu wengine na kumtukana Mungu, watu hao hawawezi kuwa na furaha, maana wako mbali na upendo na faraja za Mungu Baba! Na aliangalisha katika matunda ya rushwa , na wale ambao wanaishi kwa mapato ya biashara ya binadamu au kwa nguvu kazi ya watumwa akisema kwamba , hata kama wanapata fedha za kutosha ndani mwao hawana furaha kamili! Wao hawana hofu ya Mungu. Vivyo hivyo hata wale wanao tengeneza silaha kwa lengo la kuchochea vita ... watu ambao wanasema hawana haja ya kuja kusikia Neno la Mungu, na badala yake wanazalisha kifo, wote hao hawana Ibada kwa Mungu , ndiyo maana wanafanya biashara hizi za kifo. Kumcha Mungu, hutufanya kuelewa kuwa siku moja, tutatakiwa kutoa hesabu ya maisha yetu kwa Mungu.

Papa alikamilisha Katekesi yake na Zaburi ya 34 ambayo inasema, Maskini huyu aliita, na Bwana alisikia kilio chake na kumwokoa kutoka katika taabu zake zote. Malaika wa Bwana hufanya kituo karibu na wale wamchao, na kuwaokoa "(vv. 7-8). Tunaomba Bwana kwa neema yake, kuongeza sauti yetu na ile ya maskini, katika kupokea ile zawadi ya kumcha Mungu, ili tuweze kutambua, pamoja nao, maana ni kufunikwa na huruma na upendo wa Mungu, ambaye ni Baba yetu . Na iwe hivyo.








All the contents on this site are copyrighted ©.