Tunasikitika kutangaza kifo cha Kardinali Bernard Agre, kilichotokea Tarehe 9 Juni
2014, Jumatatu asubuhi. Marehemu Kardinali Agre alikuwa ni Askofu Mkuu Mstaafu wa
Jimbo Kuu la Abidjan (Ivory Coast). Amefariki akiwa na umri wa miaka 88, akiwa hospitalini
Paris,ambako alikwenda kupata matibabu. Kwa kifo chake, Chuo cha Makardinali
kwa sasa kimebaki na Makardinali 213 ambao kati yao 118 ni wapiga kura na 95 hawana
haki ya kupiga au kupigiwa kura katika kikao cha kumchagua Papa, kwa mujibu wa sheria
ya umri iliyopo.
Wasifu:Kwa kifupi, Kardinali Bernard Agre , alizaliwa Monga
, Machi 2, 1926, Jimbo Kuu la Abidjan na Baba Jean Manda na Jeanne Yomin. Alibatizwa
Septemba 2, 1932 katika Parokia ya Memni. Alipata elimu yake ya msingi katika shule
ya Mission Katoliki ya Memni 1936-1941. Kutoka 1941-1947 alihitimu masomo ya sekondari
katika seminari Ndogo ya Bingerville. Alianza masomo ya falsafa katika Seminari
Kuu ya Bingerville (1947-1948). Na alikubaliwa kujiunga na Seminari Kuu ya Quidah,
ya Dahomey (sasa Benin), 1948-1953 na kukamilisha masomo yake ya kiteolojia. Alipadirishwa
Julai 20, 1953 katika Seminari ndogo ya Bingerville. Baada ya utumishi mbalimbali
katika Jimbo lake , mwaka 1957, alijiunga na masomo katika Chuo Kikuu cha Kipapa
cha Urbaniana Roma, ambako aliipatia shahada ya uzamili mwaka 1960, katika teolojia,
na sheria za Kanisa. Alirudi Ivory Coast, na kwa miaka miwili baada ya kuwa
Paroko wa Parokia ya Notre Dame Treichville,na alifanywa kuwa Vika Mkuu wa Jimbo
Kuu la Abidjan.
Aliteuliwa kuwa Askofu wa Man Abidjan , Juni 8, 1968, na
kuwekwa wakfu Oktoba 3 ya mwaka huohuo, utume alioutumikia hadi Machi 25, 1992
alipoteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo jipya la Yamoussoukro, ambalo alianza kuliongoza
rasmi Mei 17, 1992. Miaka miwili na nusu baadaye, Desemba 19, 1994 aliteuliwa Askofu
Mkuu wa Abidjan. Alichukua milki ya Jimbo kuu hilo Februari 26, 1995.
Katika
ngazi ya kimataifa, 1972-1996, alishika nafasi ya Mwenyekiti wa Tume ya Maaskofu kwa
ajili ya Mawasiliano Jamii, katika Baraza linalounganisha Mabaraza ya Maaskofu
ya Mkoa Maaskofu wa Afrika Magharibi (CERAO). Kutoka 1985-1991 alikuwa Rais wa
CERAO.Mwaka 1993 aliteuliwa Rais wa Kamati ya Maaskofu Pan-African kwa ajili ya Mawasiliano
Jamii (CEPACS), Na pia alikuwa Mjumbe katika Kamati ya kwa sherehe ya Jubilei Kuu
ya Mwaka 2000. Na Rais wa Mkutano Mkuu Sinodi ya Kawaida wa 10 Maaskofu (Oktoba
2001). Tangu 2 Mei 2006, alistaafu kuwa Askofu Mkuu Mstaafu wa Abidjan.
Papa
John Paul II alimteua kuwa Kardinali katika kikao cha Consistory cha a 21 Februari
2001, na kuwa Askofu Mkuu wa jina wa Kanisa la Mtakatifu Yohana Chrysostom lililoko
Monte Sacro Altovyeo alivyobaki navyo hadi kifo chake. Tunamwombea Bwana ampokeee
katika mikono yake ya uzima wa milele.