2014-06-10 06:49:26

Heri za Mlimani ni utambulisho wa maisha ya Mkristo!


Papa Francisko , Mapema Jumatatu , akihubiri wakati wa Ibada ya Misa Takatifu, katika kanisa dogo la Mtakatifu Marta ,la mjini Vatican, alilenga juu ya somo la Injili ambamo ilikuwa ni Heri zilizo fundishwa na Yesu. Jumatatu hii ilikuwa ni siku iliyofuatia mkutano wa kihistoria uliofanyika ndani ya Vatican kwa ajili ya amani , kama alivyouitisha Yeye Papa Francisko , kwa nia ya kuhimiza ujasiri wa upole katika kuishinda chuki.

Papa Francisko, amezitaja heri hizo kuwa ni sawa na kadi ya kitambulisho cha Mkristo. Na kwamba, kwa anayejiuliza jinsi ya kuwa Mkristo mwema, jibu limo katika heri zilizo fundishwa na Yesu. Yesu alizungumzia heri hizo dhidi ya wimbi la changamoto tunazo kabiliana nazo hata leo hii. ..... Heri walio maskini katika roho. Hapa Yesu anaonyesha kwamba , mali au fedha, si dhamana ya kweli katika maisha, lakini, moyo ulio tajiri, umeridhika, kwa kuwa ubinafsi hauna mahali pa kuweka neno la Mungu....Heri yao wanaoomboleza leo hii maana watafarijiwa.

Papa alifafanua kwamba, dunia inatuambia kwamba furaha na burudani ni mambo mazuri katika maisha. Na hututazamisha katika njia nyingine, hasa wakati kuna matatizo ya maradhi, au majonzi katika familia. Dunia haitaki mateso ,na huwa na mwelekeo wa kutaka kupuuza hali za uchungu, kwa kufunika funika na mambo ya mpito. Lakini ni katika tu mtu ambaye anaona mambo kama yalivyo na moyo wake kuugulia kwa uchungu kwa hali hiyo, ndiye atakayeipata furaha ya kweli na kufarijiwa. Papa alieleza na kushukuru faraja zinazotolewa na Mkombozi Yesu Kristo, aliposema, hao si wa dunia hii. Heri walio wapole, katika dunia hii aliyo jazwa na vita, mateso na chuki, wao ni wa dunia nyingine ambako hakuna vita, hakuna chuki bali amani na upole. Aliendelea a kusema, kuwa mpole katika maisha, watu wengi hufikiri mtu huyo si mjanja . Waache wafikiri hivyo, lakini kuwa mpole kwa sababu ya dhambi na machukizo yanayofanyika duniani ni kuupata urithi wa dunia hii.

Heri wao wenye njaa na kiu ya haki, katika hili, Papa alisema, , ni rahisi sana kuwa sehemu ya wala rushwa , kupitia kishawishi kwamba kila jambo ni biashara. Kila kitu ni biashara. Papa alilitazama hilo na kusema, kwa kiasi gani, haki gani imevurugwa na kusababisha watu wengi kuteseka kwa sababu ya haki. Yesu anasema: "Wamebarikiwa wale ambao wanapambana na dhuluma dhidi ya haki. Na Heri walio na huruma kwa maana wao pia watahurumiwa. Wale ambao husamehe na kuelewa makosa ya wengine. Yesu kwao alisema - heri yao ambao hujiepusha na ulipizaji kisasi.

Papa alizitazama aya hizi za Injili ya Mtakatifu Matayo 25 akisema , ni ufunguo wa kuingia katika Maisha Matakatifu ya Mkristu. Ni Maneno machache na mepesi ,na kwa ajili ya utendaji wa wote. Kwa sababu Ukristo ni dini ya vitendo: siyo tu kwa kufikiri, bali hutekelezwa kwa vitendo. Papa alieleza na kutoa mwaliko kwa wote , kuisoma tena Injili hii kwa ajili ya kupata uelewa zaidi na utendaji ulio makini zaidi kwa ajili ya kuwa watakatifu . Na alimwomba Bwana, atujalie neema ya kuelewa ujumbe wake.







All the contents on this site are copyrighted ©.