2014-06-09 09:57:27

Shukurani zatolewa kwa Papa Francisko kwa kuitisha Mkutano wa sala


Rais Shimon Peres wa Israel , na pia Rais Mahmoud Abbas wa Palestina, Jumapili wakishiriki katika Mkutano wa sala ulioitishwa na Papa Francisko, wote wawili walionyesha moyo wa shukurani kwa Papa Francisko, kwa mwaliko wake wa kuwataka wafike Vatican katika tarehe hii 8 June 2014. Lengo kuu la mkutano huu ikiwa ni kujiweka chini ya Miguu ya Bwana, Mungu mmoja, na kuomba amani kati ya Israel na Palestina na Mashariki ya kati yote. Hotuba za Marais wawili pia zilitoa shukurani kwa hotuba nzuri iliyotolewa na Papa Francisko.

Rais wa Israel, katika hotuba yake amemtaja Papa kuwa mjenzi wa madaraja ya udugu wa aman. Na pia ilirejea maombi ya Papa ,ambamo alisisitiza haja kwa kila mmoja kufanya kazi kwa ajili ya kufikia amani, hata kwa gharama ya sadaka na maafikiano, na bila kukata tamaa hata kama inaonekana kuwa ni njia ndefu kuifikia amani kamili. Lakini ni kusonga mbele na njia hiyo kwa manufaa ya sasa na kwa vizazi vipya.

Rais Peres alionyesha imani yake kwamba, ukweli, watu wote wa Israel na pia Palestina, wana hamu kubwa ya kumkumbatiana kwa amani. Na alitaja Machozi ya akina mama juu ya watoto wao waliopoteza maisha, kumbukumbu hiyo bado, inararua mioyo ya watu wenye mapenzi mema. Hivyo, iwqapo kila mmoja ana hamu hiyo, basi inakuwa ni jambo la azima kukomesha kelele za vurugu, migogoro. Rais Peres alisisitiza, watu wote wanahitaji amani. Amani yenye kuheshimiana, usawa na uhuru.

Na Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmound Abbbas, hotuba yake ilisisitiza zaidi uwepo wa utambuzi wa kweli wa amani ya haki kwa watu wa Palestina, iwe Waislamu, Wakristo na Wayahudi . Alisema wote wanataka amani na maisha ya kuheshimiana na uhuru, uhuru wenye kuwawejesha kustawi katika nchi yao na kujitegemea. Rais Abbas alieleza na kunukuu maelezo ya Mtakatifu Yohana Paulo II, aliposema, "iwapo amani itafanikishwa Yerusalemu , amani itashuhudiwa katika dunia nzima".

Kwa hiyo , Rais Abbas kwa lugha ya Kiarabu akasema, , na tumwombe Bwana, amani katika Nchi Takatifu, Palestina na Yerusalemu, pamoja na watu wake. Tunakuomba Bwana, uijalie Palestina na Yerusalemu hasa, iwe eneo la salama kwa waumini wote, na mahali pa sala na ibada kwa wafuasi wa dini tatu zinazosadiki kwa Mungu mmoja.

Katika mkutnao huu wa maombi kwa ajili ya amani Mkoa wa Mashariki ya Kati,viongozi hawa watatu Papa, Marais wa Palestina na Israel, waliufunga kwa ishara ya amani kwa kumkumbatiana kirafiki na kwa kupanda mti wa mzeituni wa amani ndani ya Bustani za Vaican, kama kumbukumbu kwa tukio hili la kihistoria.
All the contents on this site are copyrighted ©.