2014-06-07 12:06:22

Udhibiti wa fedha haramu kimataifa!


Mamlaka ya Habari za Kifedha mjini Vatican, AIF inaendelea kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kwa kuwekeana sahihi makubaliano kati yake na Uingereza, Ufaransa pamoja na nchi nyingine nne ambazo ni Malta, Romania, Poland na PerĂ¹. Mikataba hii imetiwa sahihi na Bwana Rene Bruelhart mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya habari za Kifedha Vatican wakati wa mkutano wa mwaka wa Kundi la Egmont uliofanyika hivi karibuni nchini Peru.

Mkataba huu unahusisha kitengo cha intelijensia katika nchi hizi kama sehemu ya mchakato wa kupambana na utakatishaji wa fedha pamoja na ufadhili wa vitendo vya kigaidi kati ya nchi wanachama. Kwa makubaliano haya, nchi wanachama wanaweza kubalishana taarifa za fedha kwa usiri na kwamba, Vatican inapenda kushiriki kikamilifu katika mapambano ya utakatishaji wa fedha kimataifa.

Itakumbukwa kwamba, AIF ilianzishwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI kunako mwaka 2010 kama sehemu ya mchakato wa kupambana kufa na kupona na vitendo vya utakatishaji wa fedha haramu pamoja na ufadhili wa vitendo vya kighaidi. AIF ikajiunga na Kikundi cha Egmont kunako mwezi Julai 2013, Shirika la intelinjesia kimataifa linaloshughulikia masuala ya fedha. Kwa sasa AIF inashirikiana pia na Australia, Ubelgiji, Cyprus, Ujeruman, Italia, Uholanzi, Slovenia, Hispania na Marekani.All the contents on this site are copyrighted ©.