2014-06-07 12:05:23

Askofu mkuu Hubertus Megen ateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Eritrea


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Hubertus Matheus Maria Van Megen kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Eritrea. Wakati huo huo ataendelea kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Sudan. Askofu mkuu Hubertus Matheus Maria van Megen alizaliwa kunako tarehe 4 Oktoba 1961 huko Eygelshoven. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapadrishwa kunako tarehe 13 Juni 1987.

Askofu mkuu ana shahada ya uzamivu katika Sheria za Kanisa. Alianza utume wake katika masuala ya kidiplomasia mjini Vatican kunako tarehe Mosi, Julai 1994. Amewahi kutekeleza utume wake nchini Sudan, Uruguay, Brazil, Yerusalemu, Slovachia; Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Umoja wa Mataifa zilizoko Geneva na hatimaye, Malawi.








All the contents on this site are copyrighted ©.