2014-06-05 09:05:32

Tanzia nchini Cameroon!


Askofu Joseph Befe Ateba wa Jimbo Katoliki Kribi, nchini Cameroon, amefariki dunia tarehe 4 Juni 2014 akiwa Johanesburg, Afrika ya Kusini alikokuwa anapatiwa matatibabu kwa siku kadhaa baada ya kuonekana kwamba, afya yake inaendelea kudhohofika sana. Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka hamsini na miwili!

Marehemu Askofu Joseph Befe Ateba alizaliwa kunako tarehe 25 Aprili 1962, Nkaobe, Jimbo kuu la Yaoundè, Cameroon. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapadrishwa tarehe 20 Juni 1987. Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI alipoanzisha Jimbo jipya la Kribi nchini Cameroon, akamteuwa kuwa Askofu wake wa kwanza hapo tarehe 19 Juni 2008 na tarehe 4 Oktoba 2008 akawekwa wakfu kuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki Kribi, nchini Cameroon.







All the contents on this site are copyrighted ©.