Radio Vatican ambayo ni mwanachama wa Shirikisho la Kimataifa linaloratibu matangazo
ya Radio kwa masafa mafupi lijulikanalo kama (HFCOC: High Frequnecy Co-ordination
Conference), imeridhia kushiriki katika mchakato wa kutengeneza Radio itakayokuwa
na uwezo wa kurusha matangazo yake kwa njia ya masafa mafupi wakati wa dharura na
maafa asilia.
Katika mkutano wa Shirikisho hili unaofanyika mjini Jakarta,
Indonesia kati ya tarehe 5 - 6 Juni 2014, Radio zote za kimataifa zinazorusha matangazo
yake kwa kutumia masafa mafupi zitaridhia mwaliko huu, ili kuhamasisha Jumuiya ya
Kimataifa na Jamii kwa ujumla umuhimu wa kuwa na kituo cha radio Kimataifa kitakachorusha
matangazo yake katika masafa mafupi, kikiwa tayari na vifaa vinavyoweza kutumika katika
dharura, ili kuwasaidia watu ambao wanaweza kujikuta katika maafa.
Radio Vatican
inatarajia kurusha matangazo ya dakika 30:00 ambayo yameandaliwa na BBC kwa ajili
ya lengo hili katika maeneo ya Bara la Asia katika masafa ya 2184o khz katika masaa
05:00 na saa 5:30 UTC.