Kanisa na Zingari: Kutangaza Injili pembezoni mwa Jamii, ndiyo tema inayoongoza kongamano
la kimataifa kutoka Mabaraza ya Maaskofu Katoliki na Wakurugenzi wa kitaifa kwa ajili
ya utume wa Zingari unaonza mjini Vatican kuanzia tarehe 5 hadi 6 Juni 2014 kwa kuandaliwa
na Baraza la Kipapa la wahamiaji na watu wasiokuwa na makazi maalum.
Mkutano
huu unalenga kufanya upembuzi wa kina kuhusu mikakati ya kichungaji inayotekelezwa
na Mama Kanisa kwa ajili ya Zingari, watu ambao hawana makazi maalum na kuangalia
ikiwa kama kuna uwezekano wa Kanisa kufanya mabadiliko katika mikakati yake ya shughuli
za kichungaji kwa ajili ya Zingari.
Kanisa linajiandaa kufanya kumbu kumbu
ya miaka 50 tangu Mtumishi wa Mungu Papa Paulo VI alipotembelea Pomezia na kukutana
pamoja na Jamii ya Zingari, huu ukawa ni mwanzo wa mikakati ya kichungaji inayofanywa
na Mama Kanisa kwa ajili ya Zingari walionea katika nchi 24 duniani. Ni changamoto
ya kufanyia kazi Waraka wa Kichungaji wa Baba Mtakatifu Francisko, Injili ya Furaha
"Evangelii gaudium" kwa kuendelea kusoma alama za nyakati.