Kanisa Katoliki limekuwa ni mdau mkuu katika sekta ya elimu kwani elimu ni sehemu
ya mchakato wa Uinjilishaji wa kina unaogusa mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili.
Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii,
anapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru waalimu kwa dhamana na utume wanaotekeleza
ndani ya Jamii. Anawakumbusha kwamba, kufundisha ni utume muhimu sana unaowawezesha
kuwakaribia vijana ili kuona kilichochema, kizuri na halisi!